Katibu wa Itikani na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema Mswada wa vyama vya siasa hauna lengo la kukiumiza chama chochote na sasa ndio kwanza upo kwenye maoni hivyo wadau wote waendelee kutoa maoni kwani ni haki ya kila raia kushiriki katika kutunga sheria.
Polepole aliyasema hayo Jana, January 12 wakati wa Mdahalo wa vyama vya siasa uliandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).
Aliutetea Muswada huo huku akiwataka wapinzani kutowatisha wananchi kuhusu muswada huo.
“Tusianze kutishwa katikati ya mchakato, tusianze kujenga taswira ya kukataza kuvuka mto kabla hatujafika darajani.,
“Sasa hivi tunazungumza ndiyo maana tumepewa nyaraka, tuachwe tuzungumze tusitishwe kwa kuweka kauli timilifu. Ondoa kabisa hii, isisogee karibu na ukumbi wa Bunge, ikifika huko itakuwa balaa. Itakuwa balaa umeshafika?” Alisema Polepole
Akifafanua, Polepole alisema muswada huo unaweka utaratibu utakaoimarisha vyama vya siasa kitaasisi vitakavyowapa haki wananchi ya kushiriki siasa.
“Tunapozungumzia leo hapa masuala ya fedha, tusikimbilie fedha, fedha zilimuua Yesu pia. Hata leo, lazima tuhakikishe kwamba fedha kwenye vyama vya siasa zina utaratibu mzuri. Hatuwezi kuchukulia poa masuala ya fedha kwenye utaratibu wa vyama.” Alisema
Hata hgivyo, wakili maarufu nchini, Harold Sungusia, alimpnga Polepole huku akisema Muswada huo unampa madakaka makubwa msajili wa vyama vya siasa kuliko hata Rais.
“Msajili anaweza kuamua usajiliwe au usisajiliwe, ufutwe au usifutwe, uwe mwanachama au sio, unafaa kuwa mgombea au hufai, aina gani ya elimu ya uraia inayotakiwa na nani atoe, upewe ruzuku au usipewe,” alisema Sungusia.
“Je, akimfuta uanachama Rais? Yaani msajili ana mamlaka kuliko Rais. Ni jambo kubwa la kikatiba.”
Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa aliyesema: “Hali itakuwaje siku msajili amekwenda kwao, ameandika tangazo huko kuanzia leo Rais wa Jamhuri ya Muungano si mwanachama, akatuma katika mtandao, akaenda nje ya nchi Rwanda, Burundi, Congo sasa hali itakuwaje? Nchi itakuwaje?”
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇