LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 9, 2019

MASHAURIANO YA MGOMBEA WA UPINZANI KONGO NA KAMBI YA KABILA KUHUSU KUKABIDHI MADARAKA KWA AMANI

  • Mashauriano ya mgombea wa upinzani Kongo na kambi ya Kabila kuhusu kukabidhi madaraka kwa amani
Wawakilishi wa Felix Tshisekedi mgombea mkuu wa kiti cha urais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekutana na kambi ya Rais Joseph Kabila ili kuhakikisha zoezi la kukabidhi madaraka linafanyika kwa njia ya amani nchini humo. Hayo yameelezwa na timu ya kampeni ya Tshisekedi.
Hata hivyo kambi ya Kabila imekanusha madai hayo na kusema hakuna mkutano wowote wa aina hiyo uliofanyika baina ya pande mbili baada ya uchaguzi wa Rais wa Kongo, Disemba 30 mwaka jana ambapo matokeo kamili yanatazamiwa kutangazwa baadaye wiki hii.
Uchaguzi huo unatazamiwa kuruhusu zoezi la kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia ikiwa ni mara ya kwanza tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ipate uhuru miaka 59 iliyopita.
Huku hayo yakiripotiwa, hali ya wasiwasi inazidi kuongezeka kutokana na baadhi ya wapinzani kuituhumu serikali ya Kinshasa kuwa inajaribu kuiba kura. Kuna uwezekano Kongo ikashuhudia tena machafuko kama yale yaliyoikumba nchi hiyo katika chaguzi za 2006 na 2011 iwapo matokeo hayo ya uchaguzi yatagubikwa na udanganyifu.
Kura za uchaguzi mkuu Kongo DR bado zinahesabiwa.
Wagombea watatu wanaochuana vikali kuwania kiti cha urais ni Ramadhan Shadary wa chama tawala FCC, Felix Tchisekedi wa UDPS na Martin Fayulu wa chama cha Lamuka ambaye chunguzi za maoni zilionyesha kuwa anaongoza akiwatangulia washindani wake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages