LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 26, 2019

KESI YA RAIS WA BURUNDI DHIDI YA TELEVISHENI MOJA YA UFARANSA YAAZA KUSIKILIZWA

Mahakama mjini Paris nchini Ufaransa imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza dhidi televisheni moja katika nchi hiyo ya bara Ulaya.
Katika kesi hiyo Rais Nkurunziza anadai kuwa televisheni hiyo ya Ufaransa miaka miwili iliyopita ilionyesha picha video za mauaji ya kimbari kwa madai kuwa chama tawala cha Burundi ndicho kilichohusika na mauaji hayo.
Rais Nkurunzia anasema kuwa, picha hizo za video zilizoonyeshwa na Kanali ya Tatu ya Televisheni ya Ufaransa zinadai mauaji hayo yalifanyika katika viunga vya makazi ya Rais Nkurunziza jambo linalokanushwa na serikali yay Bujumbura.
Rais Nkurunziza amekanusha vikali madai hayo na kusema kuwa, picha hizo wala si za ndani ya Burundi bali zinavyoonekana ni kama zilichukuliwa mahala fulani katika nchi za Afrika Magharibi.
Vikosi vya usalama Burundi vimekuwa vikituhumiwa kukiuka haki za binadamu
Televisheni hiyo ya Ufaransa Channel -3 ilizirusha picha hizo mwaka 2016,wakati wa uchaguzi mkuu wa Burundi, uliofuatiwa na vurugu. Ndani ya picha hizo pia ,baadhi ya watu wanaoonekana wakizungumza lugha ya Kihausa, lugha ambayo haizungumzwi Burundi.
Serikali ya Burundi imekuwa ikiandamwa na ukosoaji kutoka kwa jumuiya za kimataifa, kwa madai kukiuka haki za binadamu na kwamba, chama tawala nchini humo kina kundi la vijana linaloitwa Imbonerakure ambalo limekuwa likkifanya mauaji dhidi ya wapinzani wa serikalii. Hata hivyo serikali ya Burundi imekuwa ikikanusha vikali madai hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages