Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akisikiliza kwa makini maelezo ya Mbunge wa jimbo la Karatu (hayupo pichani) wakati wa utoaji wa taarifa juu ya upatikanaji wa Maji katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo akitoa taarifa ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso alipotembelea wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya Maji.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Karatu.
Mbunge wa Jimbo la Karatu,Wilbroad Qambalo akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso alipozungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akizungumza jambo na viongozi mblimbali wa Wilaya ya Karatu alipotembelea wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya Maji.
Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Karatu ,Theresia Mahongo mara baada ya kukagua moja ya miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Baadhi ya Miradi ya Maji katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
Anaandika Dixon Busagaga,Karatu.
WAKAZI zaidi ya 40,000 katika wilaya ya Karutu mkoani Arusha
wako kwenye hatari ya kukosa huduma maji safi na salama endapo serikali
haitafanya jitihada za makusudi za kusimamia na kulinda miundombinu ya mifereji
katika Bonde la Easi kilipo chanzo cha maji yayotumiwa na wakazi wa Karatu.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Karatu Jublet Mnyenye wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Maji ,Juma Aweso ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya
Karatu.
“Katika bonde lile la Easi kuna chanzo kimoja cha maji ya chemichemi kuna shida sana ya utunzaji wa
miundombinu , siombei lakini ikatokea bahati mbaya kile chanzo kiiafa hapa
Karatu hatutaaenea”.alisema Mnyenye.
“Kuna watu nafikiri
zaidi ya 40,000 wako pale wanategea chanzo kile na wakati huo huo lile bonde linatumiwa na wakulima kuzalisha
zao ambalo hata kwetu kama nchi linatuletea fedha za kigeni, linazalisha
vitunguu ambavyo zaidi ya asilimia zaidi ya 80 vinapelekwa Kenya.”aliongeza
Mnyenye.
Alisema kutokana na uwepo wa tatizoo la miundombinu kumekuwa
changamoto ya ugawaji wa maji hali
inayochangia sintofahamu baina ya wakulima huku akiiomba serikali kusaidia
katika kukamilisha chanzo cha maji cha Kwa Tom.
“Tumeomba mambo mengi sana na tumeeleza shida nyingi sana mimi
ningesema basi angalau ule mradi mmoja wa Kwa Tom, kwa kipindi hichi serikali ingetuangalia
kwa jicho la pekee ,ukikamilika utakuwa umepunguza shida kubwa ya maji .”alisema
Mnyenye.
Akizungumzia mradi wa maji wa Benki ya Dunia kwa vijiji 10
,Mnyenye alisema kwa wilaya ya Karatu ni kama serikali ilipoteza fedha kutokana
na mradi huo kutekelezwa chini ya kiwango licha ya kutumia zaidi y ash Bil 3.
“Katika miradi ile mpaka leo wananchi hawaoni matokeo yake
na ni mradi wa mwaka 2012 leo ni 2019 haijafanya kazi na watu wanakata tamaa,Wananchi
wameanza kukata yale mabomba na kwa bahati mbaya niseme tu wenzangu Wamang’ati wanatumia
zile kama bangili”.alisema Mnyenye .
“Sasa Wamang’ati wakishakata kipande cha bomba wanatengenezea
bangili, kwa elemu yao ni sawa kama umewawekea bomba tangu 2013 halifanyi kazi
si wacha nivae bangili angalau basi niringe na bangili maana maji siyapati”aliongeza
Mnyenye.
Alisema ipo haja ya kupitia upya mradi huo ili kuangalia
pesa zilizotolewa zisije zikapotea bure na kwamba kama kuna uwezokano
ukarekebishwa ili kupandisha asilimia 56
za sasa za upatikanaji wa huduma ya maji kufikia asilimia 80.
Naye Mbunge wa jimbo la Karatu Willy Qulwi Qambalo alisema matarajio
na mataminio ya wananchi wa Karatu ni kupata maji na kwamba kwa hali ilivyo sasa ,ndoto ya kupata huduma hiyo muhimu imetoweka na
kwamba wananchi wameanza kupoteza imani
na serikali .
Akizungumza na vingozi wa serikali ya wilaya ya Karatu
pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Maji ,Arusha (AUWSA) Naibu Waziri wa
Maji,Juma Aweso alieleza kushangazwa na Halmashauri kuwalipa fedha
wakandarasi bila ya kufanya kazi.
“Swali dogo tu najiulizaga inakuage Mkandarasi analipwa
fedha ili hiari hakuna kazi aliyoifanya ,maana yake kabla hajalipwa fedha kuna
mtu ambaye ameidhinisha ,mhandisi wa maji wa wilaya analipwa mshahara ili
kusimamia miradi ya maji na wananchi waweze kupata huduma ya maji”alisema
Aweso.
Aweso alisema miradi mingi ya maji vijijini imekuwa kama
kichaka cha kujipatia fedha za serikali
na kwamba imefikia hatua hata
muuzaji wa mbao ambaye si mkandarasi naye amekuwa akitekeleza
mradi wa maji .
“Sasa tukubaliane yafuatayo,kwanza wahandisi ambao
walitekeleza mradi wa Maji Karatu ,aliyesimamia kama alikuwepo au yupo ,awepo
pindi nitakapo rudi hapa wiki mbili zijazo na hata kama hayupo hapa karatu
,yupo eneo linguine mumpe taarifa awepo siku hiyo.”alisema Aweso.
“Na Wakandarasi waliotekeleza hii miradi ambayo imeainishwa
watatakiwa kuwepo Site ,tutaulizana na wasitume mwakilishi waje wenyewe ili
tuhoji sasa inakuaje mkandarasi unalipwa fedha halafu hakuna kinachofanyika hata
kama kilichofanyika kanyaboya ,haiwezekani.”aliongeza Aweso.
KAWAIDA.
Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akisikiliza kwa makini maelezo ya Mbunge wa jimbo la Karatu (hayupo pichani) wakati wa utoaji wa taarifa juu ya upatikanaji wa Maji katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo akitoa taarifa ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso alipotembelea wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya Maji.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Karatu.
Mbunge wa Jimbo la Karatu,Wilbroad Qambalo akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso alipozungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akizungumza jambo na viongozi mblimbali wa Wilaya ya Karatu alipotembelea wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya Maji.
Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Karatu ,Theresia Mahongo mara baada ya kukagua moja ya miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Baadhi ya Miradi ya Maji katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
Anaandika Dixon Busagaga,Karatu.
WAKAZI zaidi ya 40,000 katika wilaya ya Karutu mkoani Arusha wako kwenye hatari ya kukosa huduma maji safi na salama endapo serikali haitafanya jitihada za makusudi za kusimamia na kulinda miundombinu ya mifereji katika Bonde la Easi kilipo chanzo cha maji yayotumiwa na wakazi wa Karatu.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Jublet Mnyenye wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Maji ,Juma Aweso ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
“Katika bonde lile la Easi kuna chanzo kimoja cha maji ya chemichemi kuna shida sana ya utunzaji wa miundombinu , siombei lakini ikatokea bahati mbaya kile chanzo kiiafa hapa Karatu hatutaaenea”.alisema Mnyenye.
“Kuna watu nafikiri zaidi ya 40,000 wako pale wanategea chanzo kile na wakati huo huo lile bonde linatumiwa na wakulima kuzalisha zao ambalo hata kwetu kama nchi linatuletea fedha za kigeni, linazalisha vitunguu ambavyo zaidi ya asilimia zaidi ya 80 vinapelekwa Kenya.”aliongeza Mnyenye.
Alisema kutokana na uwepo wa tatizoo la miundombinu kumekuwa changamoto ya ugawaji wa maji hali inayochangia sintofahamu baina ya wakulima huku akiiomba serikali kusaidia katika kukamilisha chanzo cha maji cha Kwa Tom.
“Tumeomba mambo mengi sana na tumeeleza shida nyingi sana mimi ningesema basi angalau ule mradi mmoja wa Kwa Tom, kwa kipindi hichi serikali ingetuangalia kwa jicho la pekee ,ukikamilika utakuwa umepunguza shida kubwa ya maji .”alisema Mnyenye.
Akizungumzia mradi wa maji wa Benki ya Dunia kwa vijiji 10 ,Mnyenye alisema kwa wilaya ya Karatu ni kama serikali ilipoteza fedha kutokana na mradi huo kutekelezwa chini ya kiwango licha ya kutumia zaidi y ash Bil 3.
“Katika miradi ile mpaka leo wananchi hawaoni matokeo yake na ni mradi wa mwaka 2012 leo ni 2019 haijafanya kazi na watu wanakata tamaa,Wananchi wameanza kukata yale mabomba na kwa bahati mbaya niseme tu wenzangu Wamang’ati wanatumia zile kama bangili”.alisema Mnyenye .
“Sasa Wamang’ati wakishakata kipande cha bomba wanatengenezea bangili, kwa elemu yao ni sawa kama umewawekea bomba tangu 2013 halifanyi kazi si wacha nivae bangili angalau basi niringe na bangili maana maji siyapati”aliongeza Mnyenye.
Alisema ipo haja ya kupitia upya mradi huo ili kuangalia pesa zilizotolewa zisije zikapotea bure na kwamba kama kuna uwezokano ukarekebishwa ili kupandisha asilimia 56 za sasa za upatikanaji wa huduma ya maji kufikia asilimia 80.
Naye Mbunge wa jimbo la Karatu Willy Qulwi Qambalo alisema matarajio na mataminio ya wananchi wa Karatu ni kupata maji na kwamba kwa hali ilivyo sasa ,ndoto ya kupata huduma hiyo muhimu imetoweka na kwamba wananchi wameanza kupoteza imani na serikali .
Akizungumza na vingozi wa serikali ya wilaya ya Karatu pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Maji ,Arusha (AUWSA) Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso alieleza kushangazwa na Halmashauri kuwalipa fedha wakandarasi bila ya kufanya kazi.
“Swali dogo tu najiulizaga inakuage Mkandarasi analipwa fedha ili hiari hakuna kazi aliyoifanya ,maana yake kabla hajalipwa fedha kuna mtu ambaye ameidhinisha ,mhandisi wa maji wa wilaya analipwa mshahara ili kusimamia miradi ya maji na wananchi waweze kupata huduma ya maji”alisema Aweso.
Aweso alisema miradi mingi ya maji vijijini imekuwa kama kichaka cha kujipatia fedha za serikali na kwamba imefikia hatua hata muuzaji wa mbao ambaye si mkandarasi naye amekuwa akitekeleza mradi wa maji .
“Sasa tukubaliane yafuatayo,kwanza wahandisi ambao walitekeleza mradi wa Maji Karatu ,aliyesimamia kama alikuwepo au yupo ,awepo pindi nitakapo rudi hapa wiki mbili zijazo na hata kama hayupo hapa karatu ,yupo eneo linguine mumpe taarifa awepo siku hiyo.”alisema Aweso.
“Na Wakandarasi waliotekeleza hii miradi ambayo imeainishwa watatakiwa kuwepo Site ,tutaulizana na wasitume mwakilishi waje wenyewe ili tuhoji sasa inakuaje mkandarasi unalipwa fedha halafu hakuna kinachofanyika hata kama kilichofanyika kanyaboya ,haiwezekani.”aliongeza Aweso.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇