Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amefanya ziara fupi ya kukagua maboresho ya njia ya sasa ya reli na ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dodoma hadi Makutopora ikiwa ni sehemu ya kukagua na kufuatilia utekekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020.
Akiwa katika treni ya mizigo yenye kichwa cha treni aina ya 9011 Classic Diesel Electronic Ndg. Polepole ameeleza kuridhishwa na namna ambavyo treni hiyo inafanyakazi, licha ya kuwa na changamoto za miundombinu ambazo Serikali ya CCM inazifanyia kazi kwa haraka sana.
Naye Ndugu David Majula Dereva Mkuu wa Treni - Stesheni ya Dodoma amesema “kabla tulikuwa tunasafiri kwa siku 5 kwenda Kigoma na tunabadilisha injini zaidi ya mara 4 njiani ila sasa kuna mabadiliko makubwa, tunasafiri kwa siku chache zaidi na huduma zetu za treni zimeimarika kutokana na kazi inayofanywa na Serikali hii ya Magufuli”
Aidha katika ziara hiyo Ndg. Polepole ameshiriki mkutano wa wananchi kuhusu maslahi ya wananchi kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) katika Kata ya Zuzu Wilaya ya Dodoma Mjini ambapo amewataka wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kuendelea kuwa wawazi, waaminifu kwa wananchi na kuzingatia weledi katika kazi yao kwani Serikali ya CCM chini ya Ndugu Magufuli imekwisha tenga fedha za kutosha kugharimia mradi huo.
Imetolewa na
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇