LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 30, 2018

UMILIKI WA SILAHA RAIA NCHINI KENYA WAPIKU WA POLISI NA WA WANAJESHI

Serikali ya Kenya inafanya juhudi za kuwashawishi watu wanaomiliki silaha bila kibali kukabidhi silaha zao lakini juhudi za huko nyuma zimefeli kwa sababu kumiliki silaha hivi sasa imekuwa ni sehemu katika maisha ya kila siku nchini humo.
Kwa mujibu wa televisheni ya al Jazeera ya Qatar, uchunguzi mpya wa silaha ndogodogo unaonesha kuwa kuna bastola na silaha ndogo ndogo 750,000 mikononi mwa raia nchini Kenya, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko silaha kama hizo zinazomilikiwa na polisi na wanajeshi. Televisheni hiyo imewanukuu wataalamu wakisema kuwa, kuongezeka umiliki wa silaha wa raia kunaonesha wasiwasi walio nao kuhusu usalama wao.
Kwa mujibu wa televisheni ya al Jazeera ya Qatar, kuna bastola na silaha ndogo ndogo 750,000 mikononi mwa raia nchini Kenya, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko silaha kama hizo zinazomilikiwa na polisi na wanajeshi.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imetoa muda wa siku 90 kuhakikisha watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wanakabidhi silaha zao vinginevyo sheria itachukua mkondo wake. Serikali ya Nairobi imetoa muhula huo ikiwa na matumaini kuwa wanaozimiliki watazikabidhi kwa mamlaka husika. 
Hata hivyo wataalamu wanasema kuwa, wana wasiwasi iwapo mwito huo utaitikiwa na wananchi hasa katika maeneo ya mabanda na ya vijijini ambako hakuna askari wa kutosha wa serikali. Wataalamu hao wamenukuliwa na televisheni ya al Jazeera wakisema kuwa, huenda Wakenya wengi hawapendi kumiliki silaha, lakini wanahisi ni wajibu kuwa nazo kwa sababu za kiusalama na kujilinda kwani hakuna mwingine atakayewalinda.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages