LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 27, 2018

TRUMP AFANYA SAFARI YA KUSHTUKIZA IRAQ

Rais Donald Trump wa Marekani, akifuatana na mkewe Melania jana walifanya safari ya ghafla na ambayo haikutangazwa hapo kabla nchini Iraq.
Ikulu ya White House imetangaza kuwa, katika safari hiyo ambayo haikutolewa taarifa yake hapo kabla, Trump alionana na askari wa Marekani walioko kwenye kituo cha anga cha Ain al-Asad mkoani al Anbar magharibi mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Shirika la habari la Associated Press limemnukuuTrump akisisitiza kuwa hafikirii kwa namna yoyote ile kuviondoa vikosi vya nchi hiyo katika ardhi ya Iraq na kuongeza kwamba, pale itakapolazimu kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria, Washington itaitumia Iraq kama kituo cha kijeshi cha kutekelezea operesheni hiyo.
Katika safari yake hiyo ya masaa matatu, rais huyo wa Marekani hakukutana na kiongozi yeyote wa Iraq.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul-Mahdi imetangaza kuwa mazungumzo ambayo yaliyokuwa yafanyike kati ya kiongozi huyo na Trump yamefutwa kwa sababu ya kutafautiana kuhusu namna ya kufanyika kwake. Ofisi hiyo imeongeza kuwa, kwa sababu hiyo Abdul-Mahdi na Trump wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu tu. Wabunge wa Iraq wamevieleza vyombo vya habari kuwa Trump alitaka mazungumzo hayo yakafanyike kwenye kituo cha anga cha Ain al-Asad, wazo ambalo lilipingwa na Abdul Mahdi.

Trump na mkewe Melania katika picha ya pamoja na askari wa Marekani walioko nchini Iraq

Wakati ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imesema mamlaka za Marekani ziliupa taarifa kabla uongozi wa nchi hiyo kuhusu safari ya Trump, shakhsia wengi wa kisiasa na wa makundi ya muqawama nchini Iraq wamelaani safari ya kushtukiza iliyofanywa na rais wa Marekani nchini mwao, wakisema ni ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Iraq. 
Sabah al-Saadi, kiongozi wa mrengo wa Islah katika bunge la Iraq ametaka kiitishwe kikao cha dharura cha bunge, kujadili kile alichokiita ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala ya Iraq na kusisitiza kwamba, Trump anapaswa ajue kuwa, hakuna tena suala la Marekani kuikalia ardhi ya Iraq.
Safari ya Trump nchini Iraq imefanyika baada ya kiongozi huyo kutangaza kwamba, Marekani itawaondoa wanajeshi wake nchini Syria. Hii ni baada ya kupita miaka saba ya magaidi wanaoungwa mkono na Washington na waitifaki wake kushindwa kuiangusha serikali halali ya nchi hiyo.
Wachambuzi wameuelezea uamuzi huo uliotangazwa na Trump kuwa ni ishara ya kushindwa na kugonga mwamba stratejia ya Washington nchini Syria.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages