NA K-VIS BLOG/Khamisi Sharif, Z’bar
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amesema kupatikana kwa taarifa sahihi za afya kupitia mfumo unaoaminika kutatoa taarifa ni mchango mkubwa kwa Taifa katika kuandaa mipango yake ya maendeleo. Waziri Hamad ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya ukusanyaji taarifa za afya kutoka vituo vya afya vijijini kwa kutumia simu za mkononi kupitia mfumo mpya wa DHIS. Alisema
Mfumo huo mpya wa ukusanyaji taarifa utaisaidia wizara ya afya kupata taarifa muhimu na zilizosahihi kwa haraka kutoka katika vituo vya afya vya mijini na vijijini ambazo zitatumika katika maamuzi na kuongeza ufanisi wa kazi. Alisema
Nchi nyingi za Afrika ziliopo pembezoni mwa Jangwa la Sahara zinakabiliwa na tatizo la wafanyakazi wa sekta ya afya katika kupata taarifa sahihi ambapo mafunzo hayo yaliyozishirikisha nchi 23 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Marekani yatasaidia kupunguza tatizo hilo. Waziri Hamad alisema
kuwa mfumo huo kwa sasa unatumika katika mataifa mengi duniani na unarahisisha nchi moja kupata taarifa ya nchi nyengine zinazohusu masuala ya afya kupitia simu ya mkononi. Alisema
Zanzibar ni mara ya kwanza kuingi katika hatua hiyo lakini azma ya serikali kupitia wizara yake itahakikisha inapokea kwa haraka mfumo huo ili kuona unatoa tija ya kiutendaji kwa serikali na wananchi. “Katika kuhakikisha mfumo huo unakuwa endelevu nchini, lazima kutolewa mafunzo kwa wananchi mbali mbali wakiwemo wanasiasa ambao wanamchango mkubwa katika vituo vya afya vilivyomo katika majimbo yao” alisema
Waziri huyo Aidha alisema kufanyika kwa mkutano huo wa Kimataifa wa ukusanyaji taarifa kupitia mfumo wa kisasa huko Zanzibar ni fursa pekee kwa wafanyakazi wa Wizara ya Afya kujifunza na kuthibitisha hali ya utulivu na kuaminiwa kwa nchi hiyo. Akizungumza katika mafunzo hayo Prof. Cristen Mvinje kutoka Chuo Kikuu cha Oslow nchini Norway, alisema
Chuo hicho kimejikita kutoa taaluma kwa watu mbali mbali na kutafsiri kwa vitendo elimu inayotokana na tafiti zilizofanywa na wataalamu katika kuleta maendeleo.
Mshauri wa masuala ya Teknolojia anaefanyakazi zake katika Chuo Kikuu hicho Suleiman Salum Ali alisema kwa kutumia mfumo huo wafanyakazi wa Wizara ya Afya hawatakuwa na haja ya kutumia Komputa kupata taarifa za vituo vya mashamba.Alisema
Wizara itaweza kufaidika kufanya maamuzi makubwa ya uhakika kwa muda muafaka baada ya kupata taarifa sahihi kutoka vituo mbali mbali vya afya vya vijijini. Mafunzo hayo ya siku nne ya kukusanya taarifa za afya kutoka vituo vya vijijini kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Oslow na Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇