LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2018

NANIA TAMRITHI KABILA BAADA YA UCHAGUZI WA JUMALIPIIJAYOCONGO DR?

Uchaguzi wa Rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo na utakuwa wa kwanza kuwezesha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini humo baada ya miongo kadhaa ya tawala za kidikteta, mapinduzi na mapigano ya ndani.
Hata hivyo matokeo ya uchaguzi huo ambao umesubiriwa kwa kipindi kirefu kwa ajili ya kuainisha mtu atakayechukua mikoba ya Rais Joseph Kabila bado ni kitendawili kutokana na kampeni za uchaguzi zinazotawaliwa na machafujo, ukandamizaji dhidi ya mikutano ya vyama vya upinzani na kuchomwa moto ghala la kuhifadhia vifaa vya kupigia kura mjini Kinshasa wiki moja iliyopita.
Ripoti zinasema Emmanuel Ramazani Shadary anayeungwa mkono na Rais Kabila anakabiliwa na kibarua kikubwa kutoka kwa wapinzani wake wawili kutoka vyama vya upinzani ambao ni Felix Tshisekedi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani na Martin Fayulu, mfanyabiashara na mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Exxon Mobil.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa mwezi Oktoba na kundi la Congo Research Group (CRG) la Chuo Kikuu cha New York ulionesha kuwa, viongozi wa kambi ya upinzani walikuwa wakiongoza kwa karibu asilimia 70 ya kura. Felix Felix Tshisekedi aliwatangulia wenzake kwa kupata asilimia 36 mbele ya muitifaki wake wa sasa, Vital Kamerhe aliyepata asilimia 17 ya kura.
Felix Tshisekedi
Mgombea wa chama tawala cha People's Party for Reconstruction and Democracy (PPRD) Ramazani Shadary anayepigiwa debe na Rais Joseph kabila alishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 16 ya kura akifuatuwa na Martin Fayulu aliyeshika nafasi ya nne.
Wagombea 21 ambao wengi ni wakosoaji wakubwa wa serikali ya Rais Kabila watachuana katika kinyang'anyiro hicho, suala ambalo linatishia kupunguza kura za kambi ya upinzani na kumpa matumaini mema mgombea wa chama tawala, Ramazani Shadary.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages