LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 6, 2018

MAHAKAMA YA RWANDA YAWAACHIA DIANE RWIGARA NA MAMA YAKE ADELINE RWIGARA

Mahakama mjini kigali, Rwanda imetangaza kwamba mwanasiasa Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara hawana hatia na kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.


Mahakama imesema kwamba imefanya uamizi huo kutokana na kwamba upande wa mashitaka haukutoa ushahidi wa kutosha.

Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Muendesha mashtaka alikuwa ameomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela.

Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa. Marekani imeishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo, lakini Rwanda imejibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe.

Uamuzi huo ulikuwa wa mwisho kuhusu maombi ya upande wa mashitaka ya kuwapa kifungo cha miaka 22 jela katika kikao cha mwisho mwezi uliopita, huku upande wa mawakili wao wakipinga maombi hayo na kusisitiza wateja wao kuachiwa huru mara moja.

Waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini.

Kadhalika Diane Rwigara na Mamake walishitakiwa kuchochea chuki na kusambaza uvumi kwa lengo la kuhamasisha umma kugoma dhidi ya utawala.

Uamuzi wa leo ulisubiriwa kwa hamu  baada ya Diane Rwigara na mamake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hii wakiwa hawako kizuizini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages