LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 4, 2018

MADAKTARI WAJIUNGA NA MGOMO NCHINI ZIMBABWE KUTAKA HALI BORA

Sekta kuu ya madaktari wa hospitali za uma wamejiunga na mgomo nchini Zimbabwe wakati nchi hiyo hivi sasa ikijipapatua kutoka katika mgogoro wa kiuchumi.
Hii ni mara ya pili kwa madaktari wa hospitali za uma kufanya mgomo nchini Zimbabwe mwaka huuu kupigania kuongezewa mishahara yao, huku Rais Emmerson Mnangagwa na serikali yake ikiendelea kupigania kutatua matatizo mengi ya kiuchumi. Bei za bidhaa zimepanda sana katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika sambamba na kuadimika mahitaji muhimu, madawa na mafuta.
Mathabisi Bebhe, katibu mkuu wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Zimbabwe ambacho kina wanachama 1,000 alisema jana Jumatatu kuwa, madaktari wengi wapya wamesimamisha kazi zao katika hospitali tano kuu za nchi hiyo wakilalamikia mishahara midogo, kukosekana marupurupu pamoja na uchache wa madawa. Siku chache zilizopita pia, maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani walifanya maandamano ya kupinga serikali mjini Harare Zimbabwe mbele ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo.
Maandamano ya wapinzani nchini Zimbabwe
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, maandamano hayo yalifanyika siku Alkhamisi ambapo waandamanaji walikuwa wamebeba mapango yaliyo dhidi ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walilalamikia udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na kumtaka Rais Mnangagwa ajiuzulu na utendeke uadilifu nchini humo.
Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe alilazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba 2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Mnangagwa katika uchaguzi mkuu. Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, Mnangagwa aliahidi kuleta ustawi wa kiuchumi nchini humo. Hata hivyo wapinzani wanasema kulifanyika udanganyifu na uchakachuaji mkubwa wa kura kwenye uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages