LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 14, 2018

GAVANA WA BENKI KUU PROFESA LUOGA AWATAKA WAFANYAKAZI WOTE WA MABENKI KUFANYIWA VETTING


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Profesa Florens Luoga amesema benki hiyo kama msimamizi wa mabenk nchini, itapanua wigo wake wa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) katika kupata watumishi wote wa mabenki.
Profesa Luoga ameyasema hayo jijini Dodoma leo Desemba 14, 2018 wakati akifunga semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha.
“Huwezi ukawa meneneja wa benki kama sisi hatujakuruhusu kuwa meneja wa benki, kama nilivyosema ili uwe katika uongozi wa benki lazima uwe mwaminifu otherwise tutapata all the crooks around the world (watu wote wasio waaminifu na wahalifu duniani) watakuja ku manage (kuongoza) benki za kwetu hapa wataiba kila kitu kitakwenda na hiyo tumeishaiona inatokea kwa hiyo lazima tuhakikishe kuwa menejimenti ya benki na staff wa benki lazima tuwafanyie vetting” Alisema na kuongeza
Na Sio tu kuwafanyia vetting tu sasa tutaanzisha na mafunzo ya Certification, ukitaka kufanya kazi benki lazima upitie mafunzo ambayo tutakuwa tunayaratibu ili crooks wasikae huko wanaiba tena wanaiba kweli kweli.” Alisema Profesa Luoga.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages