LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2018

CCM YAWASAMEHE MADABIDA NA WENZAKE, YAWAREJESHEA UANACHAMA, MSAMBATAVANGU YAMUWEKA UANGALIZINI

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akimshukuru Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli baada ya yeye na wenzake watatu kurejeshewa uanachama wa CCM katika kikao cha NEC, leo.

CCM Lumumba, Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaan Ranadhani Madabida na wenzake watatu  ambao walifukuzwa uanachama baada ya kupatikana na hatia ya kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Wengine ni aliyekuwa Mwenyeki wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Izengo Kwirasa,  Christopher Mwita Sanya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara na Salum Kondo Madenge ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally, amesema msamaha huo umefuatia Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kauli moja kupokea maombi ya msamaha ya Madabida na wenzake hao na kuridhia msamaha huku ikiamua kumuweka katika uangalizi Jesca Msambatavangu ambaye ameomba kurejeshewa uanachama wa CCM baada ya kufukuzwa kwa makosa ya kimaadili.

Mbali na hatua hiyo, katika kikao hicho  kilichofanyika leo chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli, Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa katika nafasi hizo kupangiwa majukumu mengine ya Kiserikali au kufariki dunia pamoja na mgombea wa CCM wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam. 

Dk. Bashiru amesema, waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dk. Damas Mukasa Kashegu,  Asha Juma Feruzi, Galila Ramadhani, Wabanhu Makene na Pamella Boniphas.

Wengine ni  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dk. Abel Mwendawile,  Aman Said Mwamwindi, Sabas Vitus Mushi Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Simiyu, Mashaka Abeid Makongoro Mayunga, Genga Ngokolo Heri na Mchunga Zebedayo.

 Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mwanza Bahebe Emmanuel Ezekiel, Nyiriza Makongoro Nyiriza, Masso Gerald, Jane Misogalya, Isaac Kilangi Kassile, Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mwanza Salum Mohamed,  Chima Yusuph, Mwandami Gwayaka, Bertha Peter, Nakomolwa Philemon na Josephat Kiemi.

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Amina Ally Kobo, Lemmy Joel Ludovick, Hamidi Rajabu Shebuge.

Pia  Halmashauri Kuu ya CCM imemteua. Abdallah Ally Mtolea kuwa Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Dk. Bashiru amesema, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeiagiza Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kurudia mchakato wa kupendekeza majina ya mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa NEC huku kwa kauli moja ikitupilia mbali pingamizi zilizowekwa dhidi ya viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali na kuagiza viongozi hao waendelee na nyadhifa zao.

Dk. Bashiru amesema , pingamizi hizo ziliwekwa dhidi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Anthony Mwandu Diallo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Lindi  Aisha Ally, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Salim Mohamed na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara George Jackson Rubagora.

Amesema, pamoja na kutupilia mbali pingamizi hizo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewaagiza walezi wa mikoa yote ambayo viongozi wake waliwekewa pingamizi wakutane na wanachama na kukiunganisha chama. 

"Halmashauri Kuu ya CCM imemuagiza Ndg. Zubeir Majaliwa (aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Uvinza) ambaye Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Uvinza ilimsimamisha uanachama kuwasilisha rufaa yake kuanzia ngazi husika wakati adhabu yake ikiendelea", amsema Dk Bashuru.

Aidha amesema Halmashauri Kuu ya CCM imetoa adhabu ya karipio kwa mwanachama wa CCM Hasnain Murji kutokana kukabiliwa na makosa ya kimaadili. 

"Kikao hicho kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na taarifa ya chama juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya mwaka 2015. 

Pia, kikao hicho kimepokea taarifa kuhusu masuala ya maadili, kimepokea na kuridhia marekebisho ya kanuni mpya za fedha na mali za chama na jumuiya zake na kimepokea na kuridhia uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM" amesema Dk. Bashiru.


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages