LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 28, 2018

CCM Blog Update: DONDOO YA YALIYOSEMWA NA RAIS MAGUFULI JUU YA KIKOKOTOO IKULU, LEO

Rais Dk. John Magufuli (pichani), amesema, Mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa coordinated, waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani.

Kwenye Baraza la Mawaziri tulikubaliana kuunganisha mifuko ya jamii, hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iunganishwe Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko.

"Mimi nataka niongee sincerely siko hapa kuwafrastrate wafanya kazi.. Nimewasikiliza, kimsingi jambo hili lina umuhimu na ndio maana nimeona niwaite. Kwa sababu nimekuwa nikisikiliza maelezo hata ya regulator, yanakuwa too academic.

Mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa coordinated, waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani.

Kwenye Baraza la Mawaziri tulikubaliana kuunganisha mifuko ya jamii, hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iunganishwe Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko.

Tulipoingia madarakani tulikuta serikali haijachangia mifuko ya hifadhi ya jamii, ikawa inadaiwa shilingi trilioni 1.23. Hivyo hata waliokuwa wanastaafu wakati ule, kuwalipa ilikuwa ngumu. Hadi Machi 2017 tayari tulishalipa deni lote hilo.

Mnafahamu mifuko hii ilikuwa inaendeshwa mingine kiajabu ajabu,
ikaanzishwa miradi ya ajabu, mingi ikiwa ya ujenzi na ni kwasababu ilikuwa ina “ten percent”, ukiangalia mradi wa Dege pale Kigamboni unawaza alitegemea “return” ya namna gani.

Mawaziri, Wabunge wanachukua hela yao yote, halafu uwaambie utachukua kidogo kidogo kila ukija, hawatakubali, kwenye reality, hata mimi hainingii.

Walioweka formula hii ni makatibu wakuu wa wakati ule, wa wakati wangu hawawezi, kwa sababu kwenye ile mifuko wengine ni beneficiary, ni kosa walifanya.

Mishahara mingi ya Wafanyakzi Serikalini si mizuri, anapofika mwisho unampa kidogo kidogo haingii, si unipe tu yote nikafie mbali, nilipokuwa nachangia hukuniambia, leo nachukua unaniambia nachukua kidogo, hata logic haingii.

Kwanza niombe kwenye mifuko, waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa, nina uhakika kama tumekuwa na wafanyakazi hewa, mishahara hewa , wanafunzi hewa, basi kuna wastaafu hewa.

Mwalimu aliyefundisha kwa uaminifu miaka 40 hadi chaki zimemharibia macho na aliowafundisha wamekuwa na mishahara mikubwa na wengine ndio Wakurugenzi wa NSSF..Ukitaka kuchukua mafao yake unamwambia nitakupa kidogo ili ukaishi, aliyekwambia nani ataishi?" amesema Rais Dk. Magufuli.

Sorce: Darmpya blog update

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages