Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mererani Wilayani Simanjiro.
Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.
“Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.
Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.
Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki kabla ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇