Na Bashir Nkoromo
Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umeandaa Kongamano maalum kubwa la kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Pombe Maguli kwa kusimamia vizuri na kwa umahiri mkubwa utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015/2020.
Katibu Mkuu wa UWT Mwalim Queen Mlozi (pichani), amesema Leo kwamba katika Kongamano hilo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa UWT Ndugu Gaudentia Kabaka na litafanyika Novemba 17, 2018 kwenye ukumbi wa PTA uliopo katika Viwanja vya Sabasaba, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozo na watu mbalimbali mashuhuri na zitatolewa mada mbali mbali kufanikisha Kongamano hilo ambalo amesema litakuwa la aina yake na la kipekee.
Katibu Mkuu hiyo wa UWT amewataka wanachama wa CCM na wananchi Kwa jumla kuhudhuria Kongamano hilo ambalo litaanza saa tatu asubuhi Kwa shamrashamra mbalimbali.
Your Ad Spot
Nov 14, 2018
Home
Unlabelled
UWT YAANDAA KONGAMANO KUBWA KUMPONGEZA MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI
UWT YAANDAA KONGAMANO KUBWA KUMPONGEZA MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇