LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 12, 2018

RAIS MAGUFULI: KOROSHO ZOTE KUNUNULIWA NA SERIKALI KWA BEI YA SH. 3,300 KWA KILO


Rais Dkt. John Pombe Magufuli  amegoma kuyauzia makampuni Korosho kwa madai kwamba ni wababaishaji na wanataka kuwaibia wananchi.
Badala yake amesema kwamba serikali itanunua korosho  yote kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.
Awali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya sh. 3000

Aliyataja makampuni hayo kuwa  ni Mega movers  ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja. 

Ombi hilo limekataliwa na Rais Magufuli kwa madai kwamba  wafanyabiashara hao  ni wababaishaji, hivyo korosho yote itanunuliwa na serikali kwa sh 3,300 kwa kilo isiyobanguliwa.

“Hawa wanaokuja leo hawa ni ujajnja tuu kwanini hawakuja mwezi uliopita? watakuja Na macondition ya ajabu. Sisi hatuwezi kukaa kimya wakulima wetu wananyanyaswa. TANTrade muanze kutafuta masoko ya mazao mengine kama cocoa Na mengine”.  Amesema Rais Magufuli

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages