LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2018

NAIBU WAZIRI WA UJENZI ANUSURIKA KIFO AJALINI

Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (pichani) leo Jumapili Novemba 11, amenusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.


Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.

“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages