LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 1, 2018

MBWA SASA WAWEZA KUGUNDUA VIJIDUDU VYA MARALIA KWA KUNUSA NGUO AU SOKSI ALIZOVAA MGONJWA

Na Bashir Nkoromo na Mitandao ya habari
MBWA waliopata mafunzo kutoka kwa wanasayansi nchini Uingereza, wanaweza kubaini vijidudu vya ugonjwa wa malaria kwa kunusa nguo au soksi alizovaa aliyeathirika.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kwenye mitandao ya Kimataifa, wanasayansi hao wamesema, ugunduzi huo mpya utasaidia sana kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa malaria na pia kuutokomeza kabsa.

Habari hizo zimesema, hatua hiyo ya mbwa kubaini vijidudu vya maralia akwa kunusa nguo au soksi za mgonjwa, ni mafanikio ya wanasayansi hao ambao bado wapo katika hatua ya awali ya utafiti unaoweza kuwapatia mwanga zaidi wa kugundua njia mpya ya kupima ugonjwa wa malaria.

“Hii ni mara ya kwanza kwa mbwa hawa wa kunusa, kufundishwa namna ya kunusa na kutambua vimelea vya malaria kupitia nguo na soksi na tumekuwa na matokeo chanya ”, Mtendaji Mkuu wa Mbwa wa tiba wa kunusa Dk. Charles Guest amekaririwa akisema wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti huo wa kwanza duniani wa kuwafundisha mbwa kunusa vimelea vya malaria kupitia nguo au soksi, wakati wa mkutano wa mwaka wa wanasayansi wa Chama cha dawa za kitropiki mjini New Orleans.

Kama ilivyoripotiwa, Mbwa tiba wa kunusa (Medical Detection Dogs), taasisi binafsi (NGO) yenye makao yake makuu nchini Uingereza, mbwa hao Labrador-Golden Retriever cross, Lexi na Labrador, Sally, waliweza kwa usahihi kabisa kutambua kwa asilimia 70 sampuli za maambukizi ya malaria na asilimia 90 ya sampuli ambazo hazikuwa na vimelea hivyo vya malaria.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages