LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2018

MBUNGE WA CUF TEMEKE, ABDALAH MTOLEA AOMBA KUJIUNGA CCM

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza wakati aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF  Abdalah Mtolea kushoto) akiomba ridhaa ya kupewa uanachama wa CCM, baada ya kutangaza Bungeni, kujiuzulu Ubunge mjini Dodoma, leo.
---
Na Mwandishi maalum, Dodoma
Wakati tarehe ya mwisho ya kupokea viongozi wa upinzani wanao omba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikifika leo hii, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama cha CUF Abdalah Mtolea amejivua uanachama wa CUF na kujiuzuru Ubunge wa Jimbo la Temeke, huku akieleza kuwa sababu ni migogoro isiyoisha katika Chama cha CUF kwa zaidi ya miaka miwili sasa. 

Mapema leo Mtolea akiwa Bungeni alitangaza kujiuzulu Ubunge wakati akichangia mjadala uliokuwa unaendelea baadae jioni hii,  aakatangaza kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, Mtolea ameeleza sababu za kuomba kujiunga na CCM kuwa ni pamoja na kushauriwa na wapigakura wake na pia kuvutiwa na Mageuzi makubwa ya kiuongozi na kazi nzuri inayofanywa na CCM na Serikali yake chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli.

Kikao hicho cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally, ambaye 
amemwelekeza kwenda katika tawi lililo karibu na makazi yake Wilayani Temeke,  Dar es Salaam ili afuate utaratibu wa kuomba uanachama wa CCM.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages