LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 16, 2018

MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA CHINA ATEMBELEA BUNGE LA TANZANIA

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto) mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto). Makamu huyo wa Rais akiambatana na Wabunge kumi na tano wametembelea Bunge la Tanzania kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
 Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng pamoja na Ujumbe wake walipotembelea Bunge mapema leo. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, Balozi China nchini Bi. WANG Ke na baadhi ya Wabunge kutoka Bunge la Tanzania na Wabunge kumi na tano kutoka Bunge la China.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng, (wa pili kutoka kushoto) Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa pili kutoka kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa kwanza kulia) na Balozi China nchini Bi. Wang Ke (wa kwanza kushoto) mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi China nchini Bi. Wang (PICHA NA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages