LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 19, 2018

MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE LA CHINA ATEMBELEA MRADI WA DARAJA LA NYERERE

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAKAMU Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. CIA DEFANG, akifuatana na ujumbe wa wabunge 16 kutoka bunge la nchi hiyo ametembelea daraja la kisasa la Nyerere linalounganisha eneo la Kurasini na Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Novemba 19, 2018. Mhe. DEFANG na ujumbe wake, pamoja na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Wang Ke, alifika eneo hilo la daraja majira ya saa 10:30 jioni na kupokelewa na Mkurugezni Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio na uongozi unaosimamia daraja hilo pamoja na wakandarasi waliojenga na kisha kupatiwa maelezo ya mradi huo mkubwa ka­­bisa hapa nchini. “Daraja hili lina urefu wa mita 680 na pia linaunganishwa na barabara yenye jumla ya kilomita 2.5, ambapo kilomita 1 iko upande wa Kurasini na kilomita 1.5 iko upande wa Kigamboni.”  Msimamizi wa Daraja hilo Bw. Emmanuel Masika alimwambia Makamu huyo Mwenyekiti wa bunge la China na ujumbe wake.
Daraja hilo lililozinduliwa Aprili 19, 2016 na Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, linamilikiwa kwa ubia ambapo Serikali inamiliki  asilimia 40% na NSSF inamiliki  asilimia 60% na limegharimu kiasi cha fedha Dola milioni 136. Aidha Bw. Masika alisema, lengo kuu la ujenzi wa daraja hilo ni kuondoa adha iliyokuwa ikiwapata wananchi ambapo walikuwa wakitegemea kivuko pekee pale Magogoni-Ferry. Aidha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio, ameshukuru kwa ujio wa kiongozi huyo, kwani ni kielelezo cha mahusiano mema na ya kihistoria kati ya China na Tanzania.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China, Mhe. CIA DEFANG, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio wakati akiwasili kwenye eneo la daraja la Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 19, 2018.
 Kiongozi wa kampuni ya Kichina iliyojenga daraja hilo, akimpatia maelezo Mhe. Defang, ya hatua mbalimbali za ujenzi wa daraja hilo. Wkawanza kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe.Wang Ke, na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio (wapili kulia). 
 Kiongozi wa kampuni ya Kichina iliyojenga daraja hilo, akimpatia maelezo Mhe. Defang, ya hatua mbalimbali za ujenzi wa daraja hilo. Wkawanza kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe.Wang Ke, na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio (wapili kulia). 
 Mkurugezni wa Uwekezaji, NSSF, Bw.Gabriel Silayo, (kulia), akibadilishana mawazo na Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo.
 Bw. Erio akizungumza na Mbunge wa Ilala Mhe. Musa Azan Zungu.
 Mhe. CIA DEFANG, alipotembelea eneo la mradi.
 Picha ya pamoja.
 Lori likielekea kwenye eneo la tozo, baada ya kupita kwenye daraja hilo.
 Msimamisi wa Daraja hilo Bw. Emmanuel Masika (kulia), akitoa maelezo ya mradi  mzima mbele ya Mhe.DEFANG.
 Sehemu ya daraja la Nyerere kama linavyoonekana ukitokea upande wa Kurasini.
  Sehemu ya daraja la Nyerere kama linavyoonekana ukitokea upande wa Kurasini.
 Kipande cha barabara ya urefu wa kilomita 1 kutoka upande wa Kurasini kuelekea darajani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages