Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Wilson Mukama akizungumza katika semina ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo katika Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Sakaam.
Akizugumza, Katibu Mkuu huyo Mstaafu, amewaasa Vijana kupigania maslahi ya Chama na sio kupigania maslahi yao binafsi huku akipinga baadhi ya viongozi ndani ya Chama wanaotambulika kama "Viongozi maslahi".
Semina ya Uongozi imeandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu ya UVCCM kwa lengo la kuwahengea uwezo zaidi viongozi was jumuiya hiyo
"Vijana rushwa ni mbaya sana, epukeni ! Ukithubutu kupewa rushwa huwezi mkosoa kiongozi huyo na hili suala la kukosoana na kujikosoa kwenye Chama chetu ni jambo mtambuka lakini twapaswa kutumia njia sahihi za kukosoana kwenye vikao na kwa kutumia lugha zenye staha" amesisitiza Mzee Mukama.
Mzee Mukama amewaeleza Vijana na Viongozi wa sasa kurejea kwenye misingi ya Chama cha Mapinduzi kule ilipotoka na amewataka kuwa na desturi ya kusoma vitabu na maandiko mbalimbali yaliyowahi kuadhimiwa na Viongozi waliopita.
Aidha, Katibu Mkuu Mstaafu Ndg.Mukama alisisitiza kwa kusema kuwa Vijana ndio wenye dhamana kubwa ya kuijenga na kuendeleza maendeleo ya Tanzania hivyo wasiogope na wala wasikubari kununuliwa.
Your Ad Spot
Nov 2, 2018
Home
Unlabelled
KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM MZEE WILSON MUKAMA AWAASA VIONGOZI VIJANA KUJIKOSOA NA KUKOSOANA KATIKA VIKAO
KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM MZEE WILSON MUKAMA AWAASA VIONGOZI VIJANA KUJIKOSOA NA KUKOSOANA KATIKA VIKAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇