Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza kuzalisha kwa wingi ndege ya kisasa ya kivita iliyopewa jina la 'Kauthar'.
Sherehe za uzinduzi wa uzalishaji kwa wingi ndege hizo imefanyika Jumamosi ya leo katika sherehe iliyohudhuriwa na Kamada Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na Waziri Ulinzi wa Iran. Ndege ya kivita ya 'Kauthar' itakuwa ya kwanza ya kizazi cha nne kutegenezwa nchini Iran.
Ndege ya kivita ya “Kauthar”, inayoruka kwa mwendo wa kasi kuliko ya sauti imeundwa kwa kutumia utaalamu wa ndani ya Iran pasina kuwepo msaada wa kigeni. Ndege hiyo ina uwezo mkubwa na ina mfumo automatiki na wa kidijitali wa kizazi cha nne. Ndege hiyo ina mfumo maalumu wa silaha na mfumo wa rubani wa HUD kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kulenga shabaha.
Ndege ya kivita ya Kauthar inayopaa kwa mwendo wa kasi zaidi kuliko wa sauti ina uwezo mkubwa wa kuzuia hujuma na uvamizi na hivyo inatazamiwa kutoa mchango mkubwa katika kuihami anga ya Jamhuri ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇