Dar es Salaam
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humpgrey Polepole (pichani) amesema Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza utolewaji wa mikopo isiyokuwa na riba ili kuwainua wananchi kiuchumi.
Amesema hayo katika kongamano la siku !bili la vijana na Uchumi lililoandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Vijana House of Vision lililofanyika kuanzia Novemba 24, 2018 katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni, Dar es salaam.
Akihutubia kwa mamia ya vijana waliohudhuria kongamano hilo Ndugu Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake itahakikisha inashirikiana Asasi za Kiraia zenye dhamira ya kuwezesha wananchi na wajasiriamali kufanikisha malengo waliojiwekea ya kuinuka kiuchumi.
"Ilani ya CCM ya uchaguzi 2015-2020 katika fungu LA 56 inazungumzia juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi hivyo lazima ipatikane namna nzuri na rahisi ya kuwawezesha wajasiriamali ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano" alisema Ndg Polepole
Polepole amesisitiza wajasiriamali kupata elimu sahihi na kuzingatia shughuli za ujasiriamali zenye tija, kutumia mtaji kidogo kwa matokeo makubwa pamoja na kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli katika kuwezesha wananchi wake kiuchumi.
Huu ni muendelezo wa Kazi Chama nje ya Chama ndani ya Jamii na katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ya CCM ya kuinua wananchi kiuchumi yanafikiwa kwa wakati
Your Ad Spot
Nov 26, 2018
Home
Unlabelled
CHAMA CHA MAPINDUZI CHASISITIZA UTOLEWAJI WA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA ILI KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI
CHAMA CHA MAPINDUZI CHASISITIZA UTOLEWAJI WA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA ILI KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇