Tunazidi kushuhudia Taifa na viongozi wetu mkichukua hatua za makusudi kubadilisha maisha ya Watanzania siku hadi siku.
Tutazidi Kumuombea Afya Njema Mhesh. Rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wote. Tunaamini mtaendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha mapinduzi pasipo kutetereka na kwa Hekima, Weledi na Uzalendo uliotukuka.
Sisi Wana CCM Diaspora ya Uingereza kamwe hatuwezi kukana, kukejeli ama kusaliti juhudi hizo.
Hivyo tunaungana na watanzania wenzetu popote walipo duniani Kuitakia Tanzania Mafanikio Mema.
Tumefuatilia kwa karibu sana katika kipindi kifupi cha miaka mitatu ni dhahiri kabisa juhudi kubwa zimefanyika zenye lengo la kuboresha hali za maisha za Watanzania kwani rushwa, urasimu na Ukiritimba vimepungua kwa kiwango kikubwa sana.
Kwa kuzingatia hayo Tunaamini Tanzania itafikia malengo ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati haraka zaidi kuliko ilivyotegemewa na hasa kama tutaanza kuwatafuta na kuunganisha vipaji na uwezo wa wazalendo wake popote walipo duniani.
Kwa nafasi hii pia tunapenda kuungana nawe kwa dhati Mhe Rais kwa hatua ulizochukua katika kushughulikia Tatizo la zao la Korosho.
Hakika umefanya uamuzi wa kimapinduzi na umefungua ukurasa mpya unaonyesha mapungufu yaliyokuwepo katika sekta yote ya mazao ya kilimo nchini. Umeendelea pia kuhamasisha wote wenye uzalendo Kuungana na kuwekeza ili Kujenga uchumi wa Viwanda, mwito ambao Sisi CCM UK Diaspora Tumeitikia Kwa vitendo. Hivyo tumeazimia Kujikita moja kwa moja katika Kuunga Mkono Kwa Vitendo Jitihada hizo.
CCM UK kwa kushirikiana na ubalozi wetu hapa London chini ya Mhesh Asha-Rose Migiro tunakuwa mstari wa mbele kuhamasisha wana diaspora kuja kuwekeza huko nyumbani hasa sekta za viwanda vidogo vinavyotumia teknolojia rahisi ili kusaidia kuhamishia uzoefu (Best practices) kwa wenzao wa huko Tanzania. Na pia tumeongeza bidii ya kutafuta masoko ya mazao kama korosho, kahawa na chai.
Kidumu chama cha Mapinduzi
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Uzalendo Kwanza
CCM-UK
Itikadi na Uenezi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇