Baadhi ya vijana ambao wanashiriki kampeni hiyo ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu ujasiriamali kupitia michezo.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
ZAIDI ya watoto 1,300 wamejuishwa katika kampeni ya kupinga
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani
Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu
ujasiriamali kupitia michezo.
Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wasichana kiuchumi uliochini
ya shirika la BRAC Anna David amewaambia waandishi wa Habari katika
viwanja vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE)
kuwa lengo la kufanya michezo hiyo kuwaleta pamoja watoto
kutoka pande mbalimbali na kuwapa elimu juu ya kupinga ukatili kwa wasichana
siku chache kabla ya kufikia maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yatakayofanyika
baadae Octoba 11 mwaka huu katika viwanja vya mwembetogwa mjini Iringa.
Bi David alisema katika maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Salum Hapi anatarajia kuwa mgeni rasmi, maamisho ambayo
siku ambayo vilevile ulimwengu unaadhimisha.
Mratibu wa mradi huo alisema waliamua kuijumuisha mkoa wa
Iringa baada ya kuona unakabiliwa na visa vya ukatili na hadi sasa
wamekwisha kuunda klabu zipatazo 50 ambazo zimekuwa zikitumika kutoa elimu ya
kupingana vitendo vya ukatili, ujasiriamali ,kuibua vipaji vya watoto
,kuwafundisha namna ya kuweka fedha na kujiajiri.
Mashindano hayo yameshirikisha watoto wa shule za
msingi,sekondari na baadhi ya watoto ambao wameshindwa kuendelea na masomo yao
kwa sababu tofauti.
Alisema kuwa kupitia michezo chini ya mwavuli wa shirika
lisilo la kiserikali la BRAC wamepeleka zaidi ya watoto 160 chuo
cha veta kwa ajaili ya kujifunza ujasiriamali.
Nao baadhi ya washiriki wa michezo hiyo Sarafina Mwinuka
alisema kuwa amepata elimu ambayo itamsaidia kuepuka na mambo yasiyofaa ikiwamo
usinzi,ndoa na mimba za utotoni.
Naye agetine Joseph na Neema Pius walisema kuwa wanajifunza
stadi mbalimbali za maisha ikiwamo kuweka akiba,kujitambua na michezo hiyo
imefanyika ikiwa wanaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kwa watoto.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇