LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 1, 2018

WAZIRI JAFO MGENI RASMI MKUTANO WA 46 WA CHAMA CHA WAUGUZI TANZANIA (TANNA)

 Mhe. Selemani Jafo, Mgeni Rasmi
Makamu Rais-TANNA, Ibrahim Mgoo akizungumza na mwaandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani 
Jafo atakuwa mgeni rasmi  katika Mkutano wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) utakao fanyika tarehe 02 hadi 05/10/2018 katika ukumbi wa  Chuo cha Mipanga kilichopo Dodoma, 

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Chama hicho Ibrahim Mgoo wakati akizungumza na mwandishi wa habari mapema leo mchana katika ofisi zilizopo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, alisema

Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2018, mkutano huo uliotanguliwa na utoaji wa huduma kwa jamii bila malipo zilizoanza tarehe 28 Septemba na kufuatiwa na Kongamano la Kisayansi kuanzia tarehe 02-05 Octoba 2018 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.Selemani Jafo ambapo zaidi ya wauguzi 1000 wanatarajiwa kufika katika mkutano huo kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara ambapo kaulimbiu: Wauguzi; Mbiu inayoongoza, Afya ni Haki ya Binadamu.
 Wananchi wakipata huduma 
Mwananchi wa Dodoma akichangia damu
 Wananchi wakisubiri huduma
 Muuguzi akitoa huduma ya upimaji wa VVU
 Mkazi wa Dodoma, Hyasinta Chuwa  akimuonesha Muuguzi, Vivienne Mchilasi baadhi ya kazi zinazo tolewa na wagonjwa wa akili baada ya kupata nafuu,  
 Afisa Muuguzi, mtaalamu wa macho Hospitali ya Msumi Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma, Gilbert Subeth  alimfanyia uchunnguzi wa macho mkazi wa Dodoma. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages