Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti 9 watakaoongoza bodi za taasisi za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao.
- Rais Magufuli amemteua Prof. Joyce L.D Kinabo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (Tanzania Food and Nutrition Centre -TFNC). Prof. Joyce Kinabo ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Chakula.
- Rais Magufuli amemteua Prof. Costa Mahalu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).
- Rais Magufuli amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Sauda Mjasiri kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (Public Procurement Appeals Authority – PPAA).
- Rais Magufuli amemteua Mhandisi Leonard Kapongo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (Public Procurement Regulatory Authority – PPRA).
- Rais Magufuli amemteua Prof. Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
- Rais Magufuli amemteua Dkt. Selemani B. Majige kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania.
- Rais Magufuli amemteua Julius Ndyamukaka kuwa Mwenyekiti wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
- Rais Magufuli amemteua Mej. Jen. Mstaafu Hamis R. Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori (TAWA).
- Rais Magufuli amemteua Prof. Romanus Cleophace Ishengoma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).
Uteuzi wa wenyeviti hawa umeanza leo tarehe 26 Oktoba, 2018.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇