16.''Rais Karia na Waziri Mwakyembe hakikisheni tunakwenda Cameroon 2019 ili mwisho wa siku mtengeneze historia kuwa mlikuwepo madarakani na Tanzania ilikwenda AFCON''-Rais Magufuli
15.''Mmekubali kuja hapa mmeingia kwenye mkataba mgumu kweli yaani nitafuatilia kila senti ya milioni 50 kujua imetumikaje na ole wao waile'' -Rais Magufuli
14."Mkifungwa na Lesotho nitajisikia aibu hata kwanini nimekuja kuwaona na kuwapa shilingi milioni 50 za walipakodi. Na najua watasema, Magufuli awatia mkosi vijana."- Rais
13.“Nitawaongezea milioni 50 na ziwe kweli kwa watu wanaotakiwa kwenda kwasababu unaeza kuta wachezaji wanaoenda kucheza ni 15 viongozi wanaenda 30, ni lazima tuiache timu iende na watu wanaotakiwa kwenda hata posho zao zitaongezeka,”Rais
12."Nilitaka kutoa ndege iwapeleke Taifa Stars visiwa vya Cape Verde, lakini ikashindikana sababu ya uwanja ulikuwa mdogo. Lakini nilipofuatilia mchezo, dakika za mwanzo tu tumefungwa magoli mawili, nikasema bora hata sikutoa ndege."- Rais
11."Ukitaka kuwa mchezaji mzuri kuna mambo ni lazima uyaache kama vile pombe, na uhuni mwingine. Ukiendekeza uhuni hutaweza kufunga magoli ya uwanjani, utafunga yale magoli mengine lakini uwanjani hutaweza kitu."- Rais
10."Viongozi wa michezo msimuingilie kocha wa timu ya taifa anayotaka kupanga, kocha ndio anayejua nani anatakiwa acheze wapi ili hata mambo yakienda sivyo tuweze kumlaumu yeye, tumpe ushirikiano na tumwache afanye kazi" Mhe Rais
9."Nilipoingia madarakani nikaona timu ya taifa inashindwa shindwa, nikawaza sijui nichukue wachezaji kutoka jeshini. Yani wao wanakuwa wanafanya mazoezi tangu asubuhi hadi usiku, akikosea anawekwa 'lockup' akitoka ni mazoezi. Lakini sasa mmeanza kunivutia"- Rais
8."Mlipopigwa yale matatu na Cape Verde mlinichukiza sana lakini angalau mkarudisha mawili hapa, napo sijafurahi sana na nimewashangaa walioshangilia maana bado tunadaiwa bao moja" Rais
7."Nataka niwaeleze ukweli; Machungu ninayoyapata mimi (kufungwa kwa Timu ya Taifa na timu nyingine) na Watanzania wanayapata"Rais
6."Niseme kwa uwazi kwamba mimi napenda michezo, lakini siyo shabiki wa timu yoyote kwa sababu kila timu ambayo nikiipenda, ikijitahidi ikakaribia mwisho, inashindwa, na mimi sipendi kushindwa"Rais
5."Nafahamu na Rais wa TFF naona na wewe umejaribujaribu kwenda vizuri, Sijui utaenda hivi hivi au nawe utaingia kwenye mtego wa wale wengine, nimeamua niseme hapa" Mhe Rais
4."Watanzania wengi wanapenda kutaja majina ya wachezaji wa nje, utakuta wanataja wachezaji wa Arsenal, Manchester na timu zingine kwasababu timu za nyumbani zinawaangusha"
3."Mnachukua tu vikombe vya hovyohvoyo na mnapongezana mara mnaitwa bungeni lakini vikombe vya maana hatujawahi kushiriki tangu enzi za mwalimu''
2."Nilikuwa nikicheza mpira nikiwa mdogo. Nilianza kwa kuwa 'forward' (mshambuliaji), lakini baadae nikapenda kuwa kipa. Nilipoanza kuvaa miwani nikaacha sababu nilijua miwani itavunjika."- Rais
1."Niseme wazi kabisa mimi nilicheza kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tatu nafasi ya Mshambuliaji lakini baadae nikawa golikipa, napenda mpira lakini naogopoa kuegemea kwenye timu moja kushabikia kwa kuwa sipendi kushindwa" Mhe Rais
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇