Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akizungumza na wazazi waliojitkeza kwenye mahafali ya shule ya msingi Kipera iliyopo kata ya Nzihi wilaya ya Iringa mkoani Iringa akiwa sambamba na mwenyekiti wa umoja wa vijana Iringa vijijini Makala mapesa katika mahafali hayo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akimkabidhi cheti kwa mwanafunzi Frola Nongele wa shule ya msingi KiperaMjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akimkabidhi cheti kwa mwanafunzi Justine Kindole wa shule ya msingi Kipera
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akiwa na viongozi mbalimbali wakielekea kukagua miundombinu ya shule ya Kipera
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele ameahidi
kumsomesha mwanafunzi wa kike atakayefaulu vizuri kwenye mtihani wa darasa la
saba katika shule ya msingi Kipera.
Kauli hiyo ameitoa hii leo
wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo iliyopo kata ya Nzihi wilaya
ya Iringa mkoani Iringa akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Akizungumza mbele ya wazazi
waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia watoto wao wakihitimu elimu ya msingi
MNEC Mtewele alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi wa kike wakimaliza
shule ya msingi wanakimbilia jijini Daresalaam kufanya kazi za ndani kinyume
cha sheria ya nchi inayotaka watoto wadogo wasome kwanza.
“Jamani mkoa wetu wa Iringa
umekuwa ukitoa wafanyakazi wengi wa ndani kwenda kufanya kazi katika miji
mbalimbali hapa Tanzania kitu ambacho kinaniumiza sana kichwa na sikipendi
kitokee tena kwa kizazi cha sasa kwa kuwa elimu inatolewa bure hivi sasa na
serikali ya awamu ya tano” alisema Mtewele
Ili kutatua tatizo hilo Mtewele
aliwaomba wazazi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wao hadi pale ambapo
wanaanza kujitegemea kwa kuwa watakuwa tayari wameshaelimika na wanauwezo wa
kufanya kazi za kuleta maendeleo kwa kutumia elimu ambayo wanayo.
Mtewele alisema kuwa atajitolea
kumsomesha mwanafunzi wa kike kuanzi kidato cha kwanza hadi chuo kikuu ambaye atafaulu
vizuri mtuhani wa darasa la saba na kumuwezesha kwenda kidato cha kwanza na
hiyo ndio itakuwa chachu ya wanafunzi wengine kufanya vizuri kwenye masomo yao.
“Ukimsomesha mtoto wa kike
unakuwa umeokoa familia yote hivyo ni lazima nitoe kipaumbele kwa mwanafunzi wa
kike ila siku nyingine nitafanya hivyo kwa mwanafunzi wa kiume lakini naomba
niwape moyo wanafunzi wote wakazane kusoma ili kujikwamia na maisha duni”
alisema Mtewele
Aidha Mtewele alichangia mifuko
arobaini (40) ya saruji kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya majengo ya shule
hiyo na kuahidi kuwa ataendelea kuwatafutia wadau mbalimbali wa kusaidia
kuiboresha shule hiyo.
Mtewele aliwaomba walimu wa
shule ya mpingi Kipera kufundisha wanafunzi kwa vitendo zaidi ili kuwaongezea
wanafunzi uelewa katika masomo wanayoyasoma ili wanafunzi wawe wabunifu katika
masomo kwa kuwa wanakuwa wanauelewa mpana wa somo husika.
Awali akisoma risala kwa mgeni
rasmi kaimu mkuu wa shule Meckzedeck Mkafule alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa
na changamotoza upungufu wa nyumba mbili za walimu,uchakavu wa nyumba tano wanazoishi
walimu wa shule hiyo .
“Walimu wengi wanaishi katika
mazingira magumu kutokana na uchakavu wa nyumba ambazo wanaishi na kusababisha
walimu kuwa na msongo wa mawazo kwa kuwa wanaishi katika mazingira magumu na
kusababisha kukosa walimu wengine ambao wanahitajika kuhamia katika shule hiyo”
alisema Mkafule
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇