LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2018

MKUU WA MAJESHI JENERALI MABEYO AKAGUA MRADI WA UJENZI WA RELI YA TRENI YA KISASA, AAMBIWA SERIKALI IMELIPA SH. BILIONI 1.35

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akioneshwa na kupewa taarifa ya namna mataluma ya ujenzi wa reli ya kisasa ya Dar es Salaam hadi Morogoro katika kijiji cha Soga, Kisarawe mkoani Pwani ambayo tayari yameshaanza kuwekwa kwenye reli.
....
Na Scolastica Msewa, Soga
SERIKALI imelipa sh. trilioni 1.35, kwa ajili ya malipo ya ujenzi wa reli ya treni ya kisasa kuanzia Dar es salaam hadi Morogoro.

Hayo yalisemwa na jana na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Treni ya Kisasa kutoka Dar es Salaam hadi morogoro, Injinia Maizo Mgedzi, wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali
Venance Mabeyo, aliyefanya ziara ya siku moja, kukagua maendeleo ya mradi huo katika maeneo ya Dar es salaam hadi Soga, Kisarawe mkoani Pwani.

Injinia Mgedzi  alisema malipo hayo ni gharama za mkandarasi wa ujenzi wa reli kwa sehemu ya Dar es salaam hadi Morogoro, yenye urefu wa kilomita 300.

Reli hiyo kutoka Morogoro hadi Makutopora, ina urefu wa kilomita 422, ambapo gharama za ujenzi ni sh. trilioni 7.02.

Alisema ujenzi huo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 28, ambapo mpaka mwezi huu, mkandarasi alikuwa na jumla ya mitambo 1,345, kati ya mitambo 727, inayotumika kwenye kazi za ujenzi moja wa moja.

Akizungumzia kazi zinazoendelea katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Injinia Mgedzi alisema ni pamoja na ujenzi wa majengo ya kambi za kwenye mradi, utafiti wa ubora wa udongo katika ujenzi wa tuta na msingi wa madaraja ya reli hiyo.

Alisema madaraja matatu yanaendelea kujengwa, ambapo tuta la reli kwa ujumla kazi imekamilika kwa asilimia 50.

Hata hivyo, alisema ujenzi katika kipande cha Morogoro hadi Makutopora, kazi zinaendelea, ikiwa ni pamoja na kuondoa udongo wa juu usiofaa, tayari kwa kujaza kifusi kizuri cha kujengea tuta, ambao umefanyika kwa kilomita 13.5.

Aidha, amewataadhalisha wananchi kujiepusha kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo la mradi, ambapo ameonya yeyote atakayehujumu miundombinu, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Tupo hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za zabuni ya manunuzi ya vichwa vya treni na mabehewa yake,” alisema Injinia Mgedzi.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mabeyo, aliomba jeshi kushirikishwa zaidi katika miradi mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini, ili lipate utaalamu zaidi, ikiwa ni pamoja na kujua njia za mawasiliano ya ndani kwa ajili ya usalama wa nchi.

Alisema fursa hiyo ya jeshi hiyo kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali, waliitafuta muda mrefu, si kwenye reli pekee, bali pia kushiriki miradi ya ujenzi wa barabara, ili jeshi hilo lipate utaalamu wa kisasa na kuwa mahiri katika ujenzi huo hapo baadae .

Jenerali Mabeyo aliongeza kuwa, jeshi hilo kushirikishwa  kwenye ujenzi huo ni sehemu ya ulinzi wa nchi.

“Jeshi hili lipo kwa ajili ya ulinzi wa taifa hili na nchi yetu ina mipaka ya kiusalama dhidi ya nchi jirani, sasa mali zilizopo nchini zinatakiwa zilindwe.

 Ikiwa umeshiriki kwenye ujenzi wa mradi kama huu, inakurahisishia zaidi kwa utendaji,” alisema.

“Ningependa tushirikishwe kwenye miradi ya kila taasisi na jeshi lishirikishwe kuanzia hatua za maandalizi ili kupata uzoefu na ujuzi, kuwezeshwa kufanya shughuli zetu za kiutendaji kiurahisi zaidi, alifafanua.

Alisema uthubfutu wa jeshi hilo kushiriki katika ujenzi unaonyesha linaweza kushiriki ujenzi wa miundombinu ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages