LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 8, 2018

MAMA ZAKIA MEGHJI AONGOZA KIKAO CHA BODI

      Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Mama Zakia Meghji akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi hiyo  mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Bodi
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya wadhamini ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt Respiciopus Boniface akifafanua jambo wakati wa kikao hicho

     Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI Mama Zakia Meghji (katikati) wakipitia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kikao hicho ,Kulia ni Mjumbe wa bodi hiyo Profesa. Bakari Lembariti na Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt, Respicious Boniface. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
    
   NA, KHAMISI MUSSA

    Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI Mama, Zakia meghji leo tarehe 08/10/2018 amewaongoza wajumbe wa bodi hiyo kupitia na kupitisha mikakati na mipango mbalimbali inayolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa kuelekea maadhimisho ya miaka 3 ya Serikali ya awamu ya 5.

   Mama Meghji amesema Taasisi ya MOI ni tegemeo kubwa kwa watanzania na nchi nyingi za Afrika hivyo ni muhiumu kuendelea ketengeneza mbinu za kimkakati za kuendelea kutoa huduma bora, kuanzisha huduma mpya za matibabu na kutekeleza kwa vitendo agizo la Mh Rais Dkt John Pombe
   Magufuli la kuhakikisha huduma zote za afya zinapatikana hapa nchini na hivyo kufuta rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo zimekua zikigharimu Serikali fedha nyingi.

“  "Nafahamu sasa tunakwenda vizuri, Serikali imetuwezesha tumekuwa na vifaa vya kisasa kabisa, tuna MRI ya kisasa sawa na ile inayotumika huko ulaya, tuna CT SCAN ya kisasa pia,tuna X-ray za kidigitali hivyo ni muhimu kuendelea kujipanga kuboresha huduma zetu ,Naamini MOI ni bora lakini ni lazima kuboresha zaidi”. Alisema Mama Meghji.
   Mama Meghji amesema pamoja na mambo mengine kikao hiki kimepitia taarifa ya mfumo wa upimaji wa wazi wa watumishi yaani OPRSAS pamoja na masuala mengine yanayolenga kuboresha huduma.

   Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema, Taasisi ya MOI iko kwenye mageuzi makubwa ya utoaji wa huduma zake hapa barani Afrika ambapo siku za hivi karibuni wananchi wengi kutoka mataifa jirani wamekuwa wakifika MOI kupata huduma, hivyo lazima huduma ziboreshwe ili waendelee kupata huduma stahiki na kwa wakati.

“  "Ni ukweli usiopingika kwamba, huduma zetu zimeboreka sana katika kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli, tuna vifaa vya kisasa  kabisa hivyo ni muhimu sisi viongozi kukutana na kuhakikisha tunaboresha huduma kadri iwezekanavyo” Alisema Dkt Boniface.

   Dkt. Boniface anasema Taasisi ya MOI imepata vifaa vya kisasa hivyo ni muhimu kukutana na kutengeneza mikakati  ya kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kwa kuleta wataalamu kutoka mataifa mbalimbali ili huduma zote ziendelee kutolewa hapa nchini ambapo hivi karibuni Taasisi ya MOI itakuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la madaktari wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.

  Vikao vya bodi ya wadhamini MOI vimekua vikifanyika kila baada ya miezi 3 kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya utoaji huduma na kuhakikisha changamoto zote zilizojitokeza katika kipindi hicho zinatatuliwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages