LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 4, 2018

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAIELEKEZA SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI DHULMA, UONEVU NA UNYANYASAJI KWA WAKULIMA KWA MANUFAA YA UCHUMI WA TANZANIA

Tarehe 03 Oktoba 2018
Katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) Mkoani Morogoro mgeni waheshima Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kimeielekeza Serikali kuendelea kudhibiti dhulma, uonevu na unyanyasaji kwa wakulima kwa manufaa ya uchumi wa Tanzania.

Akifafanua jambo hilo mbele ya wawakilishi wa vikundi vya wakulima wadogo kutoka mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar Ndg. Bashiru amesema CCM bado ni Chama Cha Wakulima na Wafanyakazi, na hivyo wakulima wa Tanzania  wasiwe na hofu, CCM  itaendelea kusimamia haki zao, kuwasemea matarajio yao na kuwa upande wao siku zote na Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli haitawaangusha.

"CCM ndio Chama cha Wakulima na Wafanyakazi... ndio Chama kinachosimamia misingi ya Mapinduzi ya Zanzibar na Azimio la Arusha... na CCM inadhamana ya uongozi... tutaendelea kukata mirija ya dhulma...uonevu na unyanyasaji kwa wakulima wa nchi hii naomba muendelee kuiunga mkono Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli haitawaangusha",  amesisitiza Ndg. Bashiru
Imeandikwa na Idara ya Uenezi CCM

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages