LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 18, 2018

ANAYETUHUMIWA KUMUUA KHASHOGGI AAGA DUNIA KATIKA AJALI YA KUTATANISHA SAUDIA


Anayetuhumiwa kumuua Khashoggi aaga dunia katika ajali ya kutatanisha Saudia

Mmoja wa watu 15 wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud, ameripotiwa kufariki dunia katika 'ajali' ya barabarani ya kutatanisha nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, Meshal Saad al-Bostani, aliyekuwa na umri wa miaka 31 na ambaye alikuwa ofisa mwenye cheo cha luteni katika Kikosi cha Anga cha Saudia huenda ameuawa ili kuvuruga zaidi ushahidi wa mauaji ya Khashoggi. 
Safu ya tahariri ya gazeti la Daily HĂĽrriyet la Uturuki limeandika leo Alkhamisi kuwa, utawala wa Aal-Saud utaua idadi kubwa ya watu ili kupotosha mkondo wa faili la mauaji ya Khashoggi, na yumkini balozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Mohammed al-Otaibi ambaye juzi usiku alitoroka Uturuki na kuelekea Riyadh akawa muhanga wa pili. 
Maafisa usalama wa Uturuki wakifanya uchunguzi katika ubalozi mdogo wa Saudia, Istanbul
Hayo yanajiri katika hali ambayo tasisi mbalimbali za haki za binaadamu duniani zinaendelea kuzishinikiza asasi za kimataifa kuuchukulia hatua kali utawala wa Aal-Saud kutokana na jinai zake tofauti dhidi ya binaadamu. 
Jamal Khashoggi alitoweka tarehe Pili Oktoba baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, siku ambayo timu ya watu 15 kutoka Saudia iliingia ubalozini hapo na baada ya saa kadhaa wakaondoka na kurejea Riyadh.
Duru za Uturuki na vyombo vya habari vilivyo karibu na serikali ya nchi hiyo vinasema mkosoaji huyo wa serikali ya kifalme ya Saudia aliuawa baada tu ya kuingia katika ubalozi huo na baadaye mwili wake ulikatwa vipande vipande.A

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages