Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo baada ya kumkabidhi jukumu kuwa msimamizi mkuu wa operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 24, 2018. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watu walionusurika katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bwisya kisiwani humo Septemba 24, 2018. Wengine ni mwananchi ambao bado wamepotelewa na ndugu na jamaa katika ajali hiyo wakisubiri kutambua miili endapo itaonekana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustine Kamuzora kwenye kijijii cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe baada ya Waziri Mkuu kutembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Nyerere kijijini hapo Septemba 24, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akikabidhi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isaack Kamwelwe mchango wa sh. milioni 10 zilizotolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama ktika kisiwa cha Ukara wilayaniu Ukerewe, Septemba 20, 2018. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara, Septemba 24, 2018.
Gari la wagonjwa likiwa limeegeshwa kwenye jengo la Kituo cha Afya cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukererwe ili kuteremsha mwili wa mtoto ambao waokoaji waliupata katika kivuko cha MV Nyerere Septemba 24, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kituo hicho leo asubuhi. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇