LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA TAASISI YA WALEMAVU



SERIKALIi imeipatia Taasisi ya Dr Reginald Mengi Foundation ( DRMF) kiasi cha Tsh Milioni 10 ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za taasisi hiyo mpya itayojihusisha katika kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu nchini.

Akikabidhi Msaada huo leo (Jumatano Septemba 26, 2018)  kwa niaba ya Serikali wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema jamii ya walemavu ni kundi mtambuka hivyo ni jukumu la wadau wa maendeleo kujitokeza katika kusaidia juhudi za Serikali katika ulinzi na haki yao.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali imendelea kutekeleza sera, sharia, miongoni na mikataba mbalimbali inayohusu haki za walemavu nchini ili kuliwezesha kundi hilo kupata huduma zote za msingi ikiwemo afya, elimu, kazi, ajira n.k

Alisema Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya kukusanya taarifa rasmi za watu wenye ulemavu waliopo katika vijiji, kata na vitongoji mbalimbali na kutambua umri, jinsia na shughuli wanazofanya.

Aidha Majaliwa alisema Serikali pia imetoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kutenga asilimia 2 ya mapato ya makusanyo ya ndani kwa ajili ya kusaidia ili kuliwezesha kundi hilo kuondokana na utegemezi wa kiuchumi pamoja na kupata mitaji ya biashara.

“Serikali itachukua hatua kali kwa Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote nchini ambaye atakikua matakwa haya ya kisheria na sasa tumeagiza pesa hizi zikusanywe na mapato yake yatangazwe hadharani kwa njia mbalimbali za matangazo ili kila mmoja ajitokeza na kupata” alisema Majaliwa.

Akifafanua zaidi Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika kutekeleza haki za kisheria na mikataba mbalimbali ya kimataifa kwa watu wenye ulemavu, Serikali imefanya mageuzi makubwa katika sekta za ajira na kazi, ambapo idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wameweza kuajiriwa nchini kupitia Sekretarieti ya Ajira na kupangiwa kazi katika taasisi mbalimbali za umma.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema Serikali pia imetoa miongozo kwa mamlaka mbalimbali za udhibiti wa  masuala ya majengo ikiwemo Bodi ya Wabunifu Majengo na Bodi ya Usajili wa Makandarasi kujenga miundombinu rafiki kwa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuwa vipando, viti, maliwato, lifti.

Aliongeza kuwa Serikali pia imekuwa ikitenga kiasi cha Milioni 6.5 na kuzipeleka katika Halmashauri mbalimbali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiwemo mafuta pamoja na vyombo vya usikivu.

Nitoe wito kwa mashirika, makampuni, taasisi pamoja na wadau wa ndani na nje ya nchi kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za Taasisi ya Reginald Mengi Foundation, kwa kuwa suala hili linagusa kila mtu katika jamii yetu” alisema Majaliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dkt. Reginald Mengi alisema Ofisi yake imepanga kutenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitachojengwa Jijini Dar es Salaam na kitakachotoa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini.

Aidha Dkt. Mengi aliitaka jamii ya watu wenye ulemavu nchini kutokata tama kwa kuwa ulemavu haimfanyi mtu kupoteza uwezo wa kufanya kazi, na badala yake aliwataka kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliyofikia.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania Mussa Kabimba alisema kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kutatoa fursa kwa watu wenye ulemavu kuwa na umoja wao utaowawezesha kuwa na sauti moja ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kiuchumi na kujiletea maendeleo yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages