LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 1, 2018

WATOTO MILIONI TANO WAMEFARIKI KUTOKANA NA VITA NA MAPIGANO BARANI AFRIKA

Watoto wapatao milioni tano wenye umri chini ya miaka mitano wamefariki dunia kutokana na vita na mapigano ya utumiaji silaha yaliyotokea katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kwenye nchi za bara la Afrika.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la kitiba na kitaalamu la The Lancet, idadi ya watoto waliopoteza maisha kuanzia mwaka 1995 hadi 2015 kutokana na vita na mapigano yaliyotokea barani Afrika ni kubwa zaidi kuliko ile iliyokadiriwa.
Jarida la The Lancet linaonyesha kuwa watoto milioni tatu kati ya milioni tano waliofariki kutokana na mapigano hayo walikuwa na umri chini ya mwaka mmoja.
Utafiti huo umebainisha kuwa kiwango hicho cha maafa kwa watoto yaliyosababishwa na vita na mapigano yaliyotokea barani Afrika hakijashuhudiwa katika bara jengine lolote lile.
Vita na mapigano husababisha pia janga la maradhi yanayoathiri zaidi watoto
Aidha idadi ya mizozo na mapigano ya utumiaji silaha yaliyotokea barani Afrika katika muda wa miaka 30 iliyopita ni kubwa zaidi kulinganisha na mabara mengine.
Watoto wadogo huwa aghalabu wanajeruhiwa katika vita na mapigano hayo na hatimaye kufariki dunia kutokana na majeraha, baa la njaa au maradhi yanayosababishwa na mizozo na kukosekana kwa amani.
Utafiti wa jarida la The Lancet aidha umeonyesha kuwa athari za mapigano ya utumiaji silaha zimekuwa zikiendelea kushuhudiwa miaka kadhaa hata baada ya kumalizika mapigano hayo na kusababisha vifo hasa kwa watoto wa nchi za bara la Afrika.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages