LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2018

WALIOFARIKI DUNIA AJALI YA MV NYERERE WAFIKA 166...SERIKALI KUTOA 500,000 KWA MWILI UTAKAO TAMBULIWA

 

Miili 116 kati ya yote iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.


Ndugu, jamaa na wananchi wamepiga kambi eneo la bandari ya Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe tangu kazi ya uokoaji ilipoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 22, mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema Serikali itatoa ubani wa Sh500, 000 kwa familia, kwa kila maiti itakayotambuliwa na kuchukuliwa kwa ajili ya maziko.

Tangu asubuhi leo, miili 30 imeopolewa na kufanya idadi ya miili iliyoopolewa hadi sasa kufikia 166 baada ya mili mingine 136 kuopolewa hadi jana jioni.

Miili yote iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages