Kituo kipya na cha kisasa cha Madaba Mkoani Ruvuma kikiwa kimewashwa rasmi usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Ujenzi wa kituo hicho ambao ulianza mwaka 2017, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea wa msongo wa 220/33kV na sasa Songea imeunganishwa na Gridi ya Taifa na tayari mitambo ya kufua umeme wa jenereta iliyoko Songea mjini imezimwa rasmi, amethibitisha Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO Bi. Leila Muhaji.
NA MWANDISHI WETU, MADABA
HISTORIA imeandikwa upya kwa wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake, baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwasha kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220/33kv cha madaba usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Kituo hicho ni sehemu ya vituo vipya vitano vilivyojengwa chini ya mradi wa umeme Makambaka- Songea.
Kwa wakazi wa Manispaa ya mji wa Songea ambao walitegemea umeme unaozalishwa kwa mashine za Jenereta, sasa wameunganishwa moja kwa moja kwenye Gridi ya Taifa, na mashine hizo zimezimwa rasmi.
Akizungumza mwanzoni mwa utekelezaji wa Mradi huo Oktoba 10, 2017, Meneja Mradi, Mhandisi Didas Lyamuya alisema, Mradi wa Makambako-Songea umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako. Lakini pia Ujenzi wa njia kuu ya usafirishaji Umeme wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilometa 245 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba na Usambazaji Umeme wa msongo wa 33kV zenye urefu wa kilomita 900 na kuunganisha wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe, Ludewa na mji wa Makambako katika Mkoa wa Njombe, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma.
Kwa maana hiyo sasa, Shime wakazi wa maeneo hayo hususan yale ya vijijni, umeme huo utakugharimu kiasi kidogo tu cha fedha kuunganishiwa nyumbani kwako, yaani sh. 27,000/= tu. Changamkia fursa hiyo ili uboreshe maisha yako kwani Mhandisi Lyamuya anasema umeme huo ni bora na wa uhakika.
Picha hii ya maktaba inaonyesha taswira ya kituo hicho cha Madaba Oktoba 10, 2017.
Katika picha hii ya Maktaba, mafundi wa TANESCO wakiwa "site' kutekeleza ujenzi wa minara yab kupitishia njia (lines) za umeme eneo la Madaba Oktoba 10, 2017. Kazin hiyo0msasa imekamilika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇