Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kulihotubia taifa siku ya leo Jumapili kwa lengo la kutoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali yanayolikabili taifa hilo la Afrika Mashariki.
Hiyo itakuwa ni hotuba yake ya kwanza, tangu zilizpozuka ghasia za kisiasa kaskazini mwa nchi hiyo mwezi uliopita katika tukio ambalo msafara wake ulirushiwa mawe.
Rais Museveni, anatarajiwa kutoa maelezo kuhusu madai ya kuhusika serikali katika kuwatesa wabunge wa upinzani na wafuasi wao wakiongozwa na Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine ambaye hivi sasa anapata matibabu nje ya nchi.
Awali Rais Museveni alikuwa amepangiwa kulihitubia taifa jana Jumamosi lakini sasa atahutubia taifa leo saa mbili usiku kwa majira ya Kampala.
Masuala mengine ambayo Rais Museveni anatarajiwa kuyazungumzia ni hatua ya wanajeshi ya kuwapiga waandishi wa habari katika maandamano yaliyotokea Kampala ya kutaka Mbunge Wine aachiliwe huru.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇