LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 30, 2018

PAMBANO LA WATANI WA JADI: SIMBA YATAWALA MPIRA KWA ASILIMIA 62% YANGA ASILIMIA 38

NA K-VIS BLOG
PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga, limemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika pambano la kwanza baina ya timu hizo la ligi kuu soka Tanzania bara lililopigwa uwanja wa taifa (Kwa Mchina)         jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2018.Hata hivyo Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo itabidi wajilaumu wenyewe kwani katika pambano hilo, walimiliki mchezo karibu dakika zote 90 ambapo Yanga walibaki wakikaba na kuokoa. Simba ilimiliki mpira kwa asilimia 62% wakati Yanga ilibaki na asilimia 38% tu.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango wao wa mchezo wa leo ilikuwa ni kujihamim Zaidi ili kupunguza madhara, na kwamba sare hiyo ni kitu kizuri kw atimu yake. 
Hata hivyo kocha mkuu wa Simba, ameisifu timu yake kwa kufuata maelekezo yake ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa kumiliki mpira ingawa bahati haikuwa yao
833A6085
Kikosi cha Timu ya Simba kilichoanza leo dhidi ya Yanga na kutoka sare ya bila kufungana.
833A6383
Beki wa Timu ya Simba, Pascal Wawa akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Heritier Makambo, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.  
833A6053
 Mgeni rasmi katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa ameongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinzia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiingia uwanjani kwa ukaguzi wa vikosi hivyo, kabla ya kuanza kwa mchezo, uliopigwa jioni ya leo kwenye Dimba ya Taifa, jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 0-0.
833A6083
 Kikosi cha Timu ya Yanga kilichoanza leo.
833A6294
 Kiungo wa Yanga, Abdallah Haji akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Simba, Mediie Kagere, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.  
833A6429
Mlinda mlango wa Timu ya Yanga, Beno Kakolanya akicheza moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake na Mshambuliaji wa timu ya Simba, Mediie Kagere, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.
833A6131
833A6141
833A6160
833A6213
833A6252
(PICHA KWA HISANI YA MTAA KWA MTAA BLOG)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages