LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2018

MUME AKIRI KUMUUA MKWEWE NA MWILI KUFUKULIWA


NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MWILI wa marehemu Celina Sulubu ,mkazi wa Lubambawe wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani umefukuliwa kwa taratibu za kisheria baada ya mumewe Selemani Hija Usumba  kukiri kumuua mkewe huyo .

Mnamo septemba 21 Usumba inadaiwa alifika kituo cha polisi Mkuranga na kuripoti kuwa mkewe Celina ametoweka nyumbani kwake tangu septemba 13 mwaka huu.

Kamanda wa polisi ,mkoa wa kipolisi Rufiji ,Onesmo Lyanga alisema baada ya kupokea taarifa hiyo mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga alifungua jalada la uchunguzi na kumshikilia kwa mahojiano na uchunguzi zaidi .


Alieleza ,katika mahojiano ya awali alikiri kumuua mkewe kwa kumkaba shingoni na kumsababishia kifo mkewe .


Lyanga alisema ,baada ya kutenda kitendo hicho aliamua kuchimba shimo kwenye shamba la jirani ambalo alikabidhiwa kulilinda na kisha kumzika .


“Mnamo septemba 22 timu ya makachero ikiongozwa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga pamoja na mashahidi mbalimbali wa tukio hili walifika eneo la tukio kwa kuongozwa na mtuhumiwa ” alifafanua Lyanga .


Lyanga alisema ,baada ya kufika eneo hilo mtuhumiwa alionyesha eneo alilozika mwili wa marehemu na kuanza kuufukua mwili huo kwa taratibu za kisheria .


Kamanda huyo alibainisha ,mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi .


Lyanga alisema ,chanzo cha tukio hili bado unachunguzwa .
Aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani nao hawatasalimika .

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages