Baada ya shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuwasha kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Madaba mkoani Ruvuma, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa amemshukuru Rais Dk. John Magufuli.
Msigwa ametoa shukrani hizo kwa niaba ya wana Ruvuma ambao ameeleza ni wazee wake kwa sababu ni mkwe wao, akibainisha kuwa adha waliyokuwa wanaipata sasa imebaki historia, kutokana na kuwa na umeme wa uhakika tofauti na zamani ilivyokuwa ambapo walikuwa wanategemea umeme wa jenereta.
"USENGWILI SANA LIDODA" Kwa tunaojua adha ambayo Songea na Mkoa mzima wa Ruvuma umepata kwa miaka mingi kutokana na tatizo la umeme, kuna kila sababu ya kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuhakikisha mradi wa kujenga njia ya umeme ya 220KV uliogharimu shilingi Bilioni 216 unakamilika. Sasa Songea imeunganishwa na gridi ya Taifa na inapata umeme wa uhakika kuliko enzi ya majenereta ambayo yalikuwa yanaelemewa mpaka yanapasuka kama ukuta wa nyumba. Kwa niaba ya Wazee wangu wa Songea, Wakwe zangu na Shemeji zangu nasema USENGWILI SANA LIDODA (Mhe. Rais), NA CHILAU MEWAWA. @ikulu_mawasiliano" Ameandika Msigwa
TANESCO ilifanikiwa kuwasha mitambo ya kituo hicho cha Madaba iliyoanza kujengwa mwaka 2017 usiku wa Septemba 13, 2018. Kituo hicho kitasambaza umeme wa kilovolti 220/33kv.
Baada ya kukamilika kwa mradi huo inakadiliwa wakazi wa maeneo hayo hususani yale ya vijiji vya karibu, wataunganishiwa huduma ya umeme kwa gharama nafuu sana kwa kiasi kisichozidi shilingi 27,000.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇