NA KHAMISI MUSSA
Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imekabidhi msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu kwa mgonjwa aliyetelekezwa na ndugu zake hospitalini hapo baada ya kukatwa miguu milili.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof, Lawrence Museru amesema kuwa hospitali imeamua kutoa msaada huo mbali na lengo la hospitali kutibu lakini pia ni kumwezesha mgonjwa kuendelea na maisha yake ya kawaida baada matibabu.
''Tumesamehe gharama zake zote za matibabu na huwa kwa wagonjwa wote wasiojiweza hospitali inadoa msaada wa matibabu, usafiri, dawa na kwa mwezi takribani hospitali inatoa msaada Tsh. 450 milioni kwa wagonjwa wasiojiweza'' amesema Prof. Museru.
Aidha Afisa Ustawi wa Jamii jengo la Kibasila, John Mwakyusa amesema kuwa Bw, Said Mtonga alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapa kwa ajili ya matibabu baada ya kusumbuliwa na miguu.
Ambapo baada ya kupatiwa matibabu aliruhusiwa kurudi nyumbani lakini ndugu zake walishindwa kujitokeza kwa ajili ya kumchukua, ndipo uongozi wa hospitali ulipoamua kumsaidia.
Kwaupande wake Bw, Said Mtonga ametoa shukrani kwa wauguzi wa wodi 11 ya Kibasila kwa jinsi ambavyo wameweza kumhudumia chakula na mavazi ambapo amesema baiskeli hiyo itamsaidia kufanya shughuli zake za kila siku.
Gharama za matibabu alizokuwa akidaiwa Mtonga tangu mwezi Mei ni Tsh. 935,824.
Tangu mwezi wa Mei hadi Septemba ambapo gharama za matunzo ziligharamiwa na hospitali
|
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇