LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 30, 2018

MAZISHI YA IGP MSTAAFU SAMWEL PUNDUGU YAFANYIKA DAR ES SALAAM


Askari Polisi wakishiriki kushusha kaburini mwili wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Samwel Pundugu, wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu Mji Mwema Kigamboni ambapo alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu,(kulia) na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati wa mazishi ya IGP mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


 Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu baada ya mazishi yake


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages