Na
Bashir Nkoromo
Shule
ya Bethel Mission iliyopo Ubungo Dar es Salaam, imepongezwa kwa
kutofelisha mwanafunzi hata mmoja kwenda Sekondari tangu kuanzishwa kwa shule
hiyo miaka 20 iliyopita.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva wakati akizungumza na uongozi, waalimu na wanafunzi katika Mahafali ya 14 ya Darasa la Saba na maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa shule hiyo.
"Ni jambo la kujivunia na linalostahili pongezi kuwa shule hii haijawahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja kwenda sekondari na matokeo yake waliokwenda mbele sasa ni wataalamu katika fani mbalimbli. hongeni sana", alisema Lyaniva.
Lyaniva aliutaka uongozi wa shule hiyo kuzingatia maslahi ya waalimu ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara inayoendana na vima vya Serikali huku akiwataka waalimu nao kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuinua hadhi ya shule hiyo.
Kwa upande wa wazazi Mkuu huyo wa Wilaya aliwahimiza kujenga tabia ya kulipa ada za watoto wao ili kuiwezesha shule hiyo kukidhi mahitaji yake ikiwemo ya kiuendeshaji.
Mapema Meneja wa shule hiyo Emmanuel Mshana alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada kwa wakati jambo ambalo alisema linafifiza juhudi za shule hiyo kufikia kwa haraka malengo inayopanga katika kuboresha huduma zake.
"Licha ya mafanikio wanayoonyesha kuwa nayo wanafunzi wanaomaliza leo lakini miongoni mwao kunaambao wazazi wao wanadaiwa ada ambapo shuleinadai Sh. Mlioni 5 ambazo kutokana na sababu mbalimbali hazikulipwa", alisema Mshana.

Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akimlaki Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alipowasili kuwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya 14 ya darasa la saba na maadhimisho ya miaka 20 ya shule hiyo, jana.
Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akitoa taarifa fupi kuhusu shule hiyo Kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwĂ sili shuleni hapo.
" Mtoto hujambo?" Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akimsalimia Mtoto aliyemkuta mlangoni wakati anatoka katika ofisi ya Meneja wa Bethel Mission School baada ya mazungumzo mafupi.
Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akisindikizwa na mwenyeji wake, Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana kwenda kwenyeviwanja vya shughuli ya mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikata utepe kuzindua maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa Kwa Bethel Mission School, alipofika shuleni hapo Kwa ajili ya maadhimisho hayo na sherehe za mahafali ya 14 ya Darasa la saba. Kushoto ni Meneja wa Shule hiyo Emmanuel Mshana na kulia ni Alvines Okuku wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwasalimia wananchi wakati akiingia kwenye Viwanja vya mahafali hayo. Kushoto ni Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana.
Wahitimu wa darasa la saba waBethel Mission School wakiingia ukumbini Kwa wimbo maalum wakati wa mahafali hayo
Wahitimu hao wakiongoza kuimba wimbo wa Taifa na wimbo wa shule hiyo
Baadhi ya waliohudhuria mahafali hayo wakiungana na wengine kuimba wimbo wa Taifa
Mkuu wa Wilaya ya Temeke akisalimia baada ya kutambulishwa Mchungaji Bright Fue (kushoto), wakati wa mahafali hayo
Mchungaji Fue akisalimia baada ya kutambulishwa na Meneja wa shule hiyo
Baadhi ya wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo
Wanafunzi wakionyesha uhodari wao katika kutoa burudani wakati wa mahafali hayo
Wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo wakioeleza kuhusu stadi za rangi
Wanafunzi wa darasa la tatu katika shule hiyo wakiimba ngonjera
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiingia ukumbini kuburudisha.
Mchungaji Fue akizungumza kwenye mahafali hayo
Kijana akionyesha chapegne kabla ya kuifungua
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva (wa tatu kushoto) akigonganisha glasi yenye kinywaji cha shampeni na walimu na wazazi wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Meneja wa shule hiyo Emmanuel Mshana.
Keki maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa shule hiyo
Mmoja wa wanafunzi waliosoma Bethel Mission School ambaye sasa ni Daktari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akikata keki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi waliosoma Bethel Mission School ambaye sasa ni Daktari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akikata keki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi waliyomaliza 2005 katika shule hiyo Elizabeth Nyalusi (kulia) ambaye kwa sasa ni mfanya biashara akimlisha kipande cha keki mama mwanzilishi wa shule hiyo, Dorothy Mseli
Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akisoma risala kwa mgeni rasmi
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza wakati wa mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi bora wa kike kitaaluma aliyehitimu darasa la saba
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi bora wa kiume kitaaluma aliyehitimu darasa la saba
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi zawadi kwa mwalimu mchapakazi wa shule hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi zawadi kwa mwalimu mchapakazi wa shule hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa drasa la saba wakati wa mahafali hayo
Wazazi wakimpongeza mtoto wao kwa kuhitimudarasa la saba katika shule hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bethel Mission School mwishoni mwa mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa katika picha ya pamoja na wahitimui wa darasa la saba wa Bethel Mission School mwishoni mwa mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa zamani wa wa Bethel Mission School mwishoni mwa mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi zawadi iliyotolewa na wanafunzi wa zamani wa Bethel Mission School mwishoni mwa mahafali hayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Bethel Mission School mwishoni mwa mahafali hayo. Picha zote na CCM Blog

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇