Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya tarafa kwa tarafa ambayo anatarajia kuianza siku ya kesho katika wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuijenga Iringa mpya yenye maendeleo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi anatarajia kuanza ziara ya kikazi kwa kuzitembelea tarafa zote 15 za wilaya zote 3 za mkoa wa Iringa lengo likiwa ni kufanya jumla ya mikutano 37 na kutembelea jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi 78,138,549,216 ambayo itausisha ukaguzi,uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mh: Hapi alisema kuwa anatarajia kutembea jumla ya kilometa 2,611 wakati wa ziara hiyo ya kikazi kwenye mkoa wote wa Iringa.
“Nitatembea tarafa tano za wilaya ya Mufindi ambazo ni Ifwagi,Malangali,Kibengu,Sadani na Kasanga,wilaya ya kilolo nitatembelea tarafa tatu ambazo ni Mazombe,Kilolo na Mahenge na kumalizia wilaya ya Iringa yenye tarafa saba ambazo ni Kalenga,Ismani,Pawaga,Idodi,Mlolo,Kiponzelo na Iringa mjini hapo ndio nitakuwa nimemaliza ziara yangu ya tarafa kwa tarafa” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuijenga Iringa mpya katika dhana ya kuboresha utendaji wa serikali,kuimarisha sekta za kilimo,ujenzi wa viwanda,utalii,miundombinu,biashara,huduma za afya,maji,elimu,utatuziwa kero za wananchi na kutengeneza fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa.
Aidha Hapi alisema kuwa atafanya mikutano mikubwa kumi na saba na midogo 20 ambapo mikutano kumi na tano itafanyika katika tarafa kumi na tano kwa kuambatana na wataalam mbalimbali kutoka idara zote za serikali na taasisi za UMMA.
“ Katika ziara yangu zitatoa sana fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kutoa kero zao kwa lengo la kutatua matatizo ambayo yanawakumba wananchi na nitawaeleza muelekeo wa kujenga Iringa mpya” alisema Hapi
Hapi aliwataka viongozi wote wa mkoa kuanzia wakuu wa wilaya haviongozi wa chini kuiga mfano wake wa kwenda kutatua kero za wananchi na wasipofanya hivyo hatakuwa na msamaa kwa viongozi wote wazembe na ambao hawatatui kero za wananchi.
Naomba kumalizia kwa kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yangu na kuhumiza viongozi wanatakiwa kuwepo kwenye ziara yangu bila kukosa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇