Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari kati Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza kimezama leo Alhamisi Septemba 20, 2018.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.
Kamanda Shana amesema kuwa kivuko hicho kimezama leo mchana baada ya kupinduka.
“Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka,” amesema.
Amesema kuwa watu watatu wameokolewa na shughuli ya uokoaji inaendelea ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo, John Mongella.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇