MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, Dkt. Misanya Bingi amefariki dunia mapema leo asubuhi Septemba 16, 2018.
Taarifa za awali zinasema marehemu Dkt.Misanya ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio One kwenye miaka ya mwanzoni ya 90, amefariki wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla.
Dkt. Misanya Bingi, Enzi za uhai wake.
Dkt. Misanya Bingi, akiwa na Abubakar Liongo. Wote waliwahi kufanya kazi Radio One kama watangazaji.
Dkt. Misanya Bingi, akilishwa keki na Isack Gamba. Wote walifanya kazi Radio One.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇